May 30, 2020



KESHO Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam majira ya saa nne asubuhi vumbi litatimka kwa mchezo wa kukata na shoka kati ya Wanahabari Waliooa na Wasiooa.

Makocha wa timu zote mbili wamemwaga tambo zao kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu ambapo Waliooa wamesema kuwa watawafundisha namna ya kucheza wapinzini wao huku Wasiooa wakisema kuwa watawakimbiza wapinzani wao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Waliooa, Katanga Omary amesema kuwa maandalizi yapo sawa kinachosubiriwa ni muda wa mchezo ili kumaliza ubishi.

"Kila kitu kipo sawa kwani wapinzani wetu wanafikiria itakuwa rahisi kupata ushindi mbele yetu hilo jambo wasahahu kwani tumejipanga na tupo tayari kuwafundisha namna ya kucheza mpira ndani ya uwanja kwani uzoefu tunao.

"Ipo wazi kwamba uzoefu tulionao unatupa nafasi ya kufanya vizuri lakini ukweli utabaki palepale wapinzani wetu watakwepa yote ila sio kichapo, tutapanga idadi ya mabao tutakayowafunga na tukimaliza tutawapa semina kuhusu majukumu wasikae macho juu juu," amesema.

Kocha Mkuu wa Wasiooa FC, Wilison Oruma amesema:- "Tupo sawa kimsingi asilimia kubwa tumekuwa na program za pamoja ambazo zinatufanya tuwe pamoja, wachezaji wapo sawa kutoa furaha kwa mabachela.

"Tunahitaji ushindi kwa kiwango kikubwa, vijana nimewaambia wana kazi mbili kubwa ya kwanza kutafuta ushindi kisha ya pili ni kutoa burudani ili mashabiki wao wafurahi, itakuwa ni kazi kubwa kweli ila tupo tayari.

"Pia tunachukua tahadhari kwani ni muhimu sana kuendelea kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona kutakuwa na elimu pia ambayo itatolewa kwa wachezaji ambao ni waandishi wa habari watapewa semina zitakazotakiwa kwenye michezo, maji tiririka na vitasa mikono ni vifaa ambavyo vitakuwepo, kila kitu kipo sawa," amesema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic