June 16, 2020


KLABU ya Arsenal imesema ipo tayari kukaa chini na staa wake, Alexander Lacazette na kujadili mustakabali wake ndani ya klabu hiyo.

Lacazette alianza msimu huu vibaya jambo ambalo lilipelekea kusugua benchi, huku nafasi yake akipewa dogo, Eddie Nketiah aliyerudi kikosini akitokea Leeds alipokuwa akicheza kwa mkopo.

Baada ya kuelezwa kuwa Atletico Madrid inahitaji saini yake, Arsenal imepanga wiki zijazo kukutana na mchezaji huyo na kufanya mazungumzo.

Arsenal kwa sasa imesema haipo tayari kupoteza mastaa wake wawili kwa pamoja wanaounda safu ya ushambuliaji ambao ni Lacazette na Pierre Emerick Aubameyang.

Mkataba wa Lacazette unatarajiwa kumalizika mwaka 2022 huku Aubameyang ukimalizika 2021.

Imeelezwa kuwa kama Aubameyang ataamua kuondoka, basi Lacazette atasalia kuwa mshambuliaji wa kati.

Ripoti zinaeleza kuwa, kama Lacazette atauzwa, basi dau lake ni pauni 60m ambazo zitaifanya klabu hiyo kumpata mchezaji wa Atletico Madrid, Thomas Partey.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic