June 30, 2020

FELIX Miziro, Kocha Mkuu wa Mbao FC amesema kuwa angekuwa kwenye kikosi hicho tangu awali timu hiyo isingepata tabu ya kuwa  kwenye presha ya kushuka daraja.

Mbao FC ilikuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco ambaye alibagwa manyanga kwa kile alichoeleza kuwa ni kutoridhika na matokeo aliyokuwa akiyapata kutokuwa mazuri.

Kwa sasa Minziro amekabidhiwa timu ambapo ameingoza kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 na amesepa na pointi sita na mabao mawili.

Mchezo wake wa kwanza aliitungua Coastal Union ya Juma Mgunda bao 1-0 kisha akamalizana na Polisi Tanzania kwa kuifunga bao 1-0.

Licha ya kushinda pointi zote sita anabaki nafasi ya 19 akiwa na pointi 29 kibindoni.

Minziro amesema:"Ningekuwa na timu hii tagu awali nina amini kwamba tungekuwa mbali, tusingekuwa hapa tulipo ila hamna namna kwa kuwa nipo wakati huu nina kazi ya kufanya ili kuona timu inabaki kwnye ligi.

"Ushindani ni mkuhwa na nilipopewa kikosi nilianza kuwanyoosha kwanza wachezaji ndio maana tulianza kwa ushindi na tumeendelea kupata ushindi hivyo ni wakati wetu kuendelea kupambana kufikia malengo yetu ya kushiriki ligi msimu ujao," amesema,

Ikiwa imecheza mechi 32 imebakiwa na mechi sita ili kukamilisha mzunguko wa pili na inatakiwa ishinde mechi zote kujihakikishia nafasi za kubaki ndani ya ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic