June 10, 2020


KIKOSI cha Yanga leo kimeanza safari ya kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui utakaochezwa Juni 14.

Katika kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa, mtupiaji namba moja David Molinga ameachwa Bongo huku habari zikieleza kuwa amegoma jambo ambalo amelikanusha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, David Molinga ameandika:- Nataka nikanushe hii habari kwamba nimegoma kusafiri na team kwanza nimewakumbushe kitu cha peke imenileta Tanzania ni mpira na kazi yangu ndio iyo sasa iko ivi tangu team imeanza mazoezi sijawahi kukosa na nafata program za mwalim vizuri.

" Lakin jana list (orodha) ilitoka na mimi jina langu halijakuwepo sasa itasemekana vipi mimi nimegoma kama ndio ivyo muulizeni coach ndio alitaja list (orodha) yake imekuwa tabia kila mara kila kitu mimi tu ata kama sjafanya kitu kibaya utaskia tu Molinga 'this is too much' (hii imezidi).

2 COMMENTS:

  1. Pole baba na uzidi kuvumilia. Ukifanya wema usitaraji kulipwa wema ijapokuwa wewe ndie mpaka sasa ulieandika mabao mengi zaidi na kamba siku zote hukatikia pabovu

    ReplyDelete
  2. Mtafute Zahera uondoke kwani Yanga mara nyingi wanadai alikuleta Zahera na si wao. Usilazimishe kubaki Yanga utacheza po pote tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic