June 30, 2020


YANGA leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Maxime itajilaumu yenyewe kipindi cha kwanza kwa kushindwa kutulia na kutumia nafasi ambazo walizitengeneza kwani walikuwa kwenye ubora upande wa kiungo wakiwapoteza mazima wachezaji wa Yanga.

Bao la Kagera Sugar lilipachikwa kiufundi na nyota wao Awesu Awesu mwenye rasta kichwani ambaye alifunga akiwe nye kidogo ya 18 akimalizia pasi ya kisigino ya Yusuph Mhilu dakika ya 19.

Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 ambapo kipindi cha pili walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ditram Nchimbi na nafasi yake ikachukuliwa na Mrisho Ngassa mwamba wa ziwa Victoria mzee wa enjoi soka.

Dakika ya 52 Molinga alifunga bao la kuweka usawa akimalizia pasi ya kichwa ya Ngassa naye akifunga bao la kichwa na kuwarudisha mchezoni Yanga.

Katika harakati za Kagera Sugar kutaka kufunga, Awesu alionekana amechezewa faulo na Metacha Mnata ndani ya 18 mwamuzi wa kati akamuonyesha kadi ya njano ya kwanza Awesu.

Yanga iliandika bao la ushindi dakika ya 76 kupitia kwa Deus Kaseke ambaye alifunga bao hilo kwa penalti baada ya mwamuzi kutafsiri kuwa alichezwa faulo Mrisho Ngassa ndani ya 18.

Awesu baadaye alionyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kile ambacho mwamuzi alitafsiri namna anavyojua ndani ya uwanja kwani tukio lilionyesha kuwa alichezewa faulo, alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje dakika ya 78. 

Kwa sasa Yanga inakula upepo ikisubiri mshindi wa mchezo wa kesho kati ya Simba ama Azam hatua ya nusu fainali.

16 COMMENTS:

  1. TFF angalieni mechi za yanga, ni aibu kwa nchi maana mechi zinarushwa live dunia inaona. Pia inaumiza timu zinazokitana hii kadhia ya waamuzi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona ile ya Simba na Yanga 4/12/2019 hawajaiangalia jinsi Kagere alivyojirusha na kupewa penati?

      Delete
  2. Kwa kweli kilichofanyika Leo taifa ni aibu kubwa. Nitashangaa Kama hao yanga watasherehekea ushindi wa kubebwa kiasi kile

    ReplyDelete
  3. Kama kuna kubebwa basi ya leo ndio babu kubwa.Penalti ya haramu faulo ilikuwa nje ya eneo la hatari.Awesu aliangushwa na kipa akapewa yeye kadi.Awesu kachezewa faulo akaonyeshwa kadi ta pili ya njano nรค kuwa nyekundu.Uonevu wa wazi kabisa.Inatia aibu kwa maendeleo ya mpira nchini Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Bora kubebwa kuliko kununua mechi. Mikia mnachofanyiwa sasa hivi ni kununuliwa mechi tu. Hamna timu. Kuna timu duniani yenye wastani wa umri miaka 30. Angalia Chama, Boco, kagere, wawa

    ReplyDelete
  5. Ata kama ingekuwa nje ya 18 tungefunga tu. Kwani ile ya Morrison tarehe 08 ilikuwa penalti?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakikujibu hilo swali tafadhali nijulishe na mie ndugu...,,๐Ÿ˜๐Ÿ˜

      Delete
    2. Lile goli la jkt lilikuwa ndani au nje ya 18?

      Delete
  6. Mikia fc mmesahau mechi ya yanga kagere alichezewa nje ikatengwa penati na magoli ya offside mechi ya polisi na namungo mnajifanya wehu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanajisahaulisha hao mbumbumbu fc

      Delete
    2. Mmesahau mlichowafanyia polisi na lipuli...mnaona zaidi ya wenzenuhata azam pia waliwalalamikia hilo hamlioni...siwashangai 7bu kuanzia timu mpaka mashabiki hamna nidhamu..malalamiko fc

      Delete
    3. Hata Namungo goli offside dakika ya 97

      Delete
  7. Utopolo hawana aibu hii mechi ya ngapi wanabebwa kuanzia namungo, azam na kageta afadhali waamuzi watoke nje ya nchi

    ReplyDelete
  8. Huwezi kuhalalisha kubebwa kwa yanga eti kwa vile unadhani na simba ilibebwa, sasa wanaoumia ni timu ndogo zinzoonewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic