June 10, 2020



CLATOUS Chama na Miraj Athuman,’Sheva’  viungo wa Simba wamepewa program matata ili kurejesha makali yao pale ligi itakaporejea.

Chama alikuwa Zambia baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona alirejea nchini Juni 7 huku Sheva yeye alikuwa nje ya uwanja tangu Desemba mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama.

Kwenye mazoezi ambayo Simba wanaendelea kuyafanya ndani ya viwanja vya Simba Mo Arena kocha wa viungo, Adel Zraine alikuwa akiwasimamia kufanya mazoezi hayo wakitumia kiwanja cha nyasi bandia.

Program ya kwanza ambayo walitumia muda mrefu kuifanya ilikuwa ni umiliki wa mpira kisha likaja zoezi la kupiga pasi na program ya tatu ilikuwa ni kulenga shabaha.

Mbali na program hizo pia walikuwa wakikimbia mbio fupi, kuruka koni pamoja na kuchezea mpira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic