CHARLES Mkwassa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kichapo cha mabao 3-0 mbele ya KMC jana umetokana na makosa yao wenyewe waliyoyafanya ndani ya uwanja.
Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa Uwanja Uhuru na ulikuwa na ushindani mkubwa tangu mwanzo wa kipindi mpaka dakika 90 zilipokamilika.
KMC iliweza kuandika mabao yake matatu kupitia kwa Sadala Lipangile dakika ya 31, Charles Ilanfya dakika ya 45 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Hassan Kabunda dakika ya 65.
Mkwassa amesema kuwa mbali na makosa madogo ambayo wameyafanya uwanjani pia hawakuwa na muda mrefu wa kuandaa kikosi katika mechi za ushindani kutokana na ligi kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.
"Hatukuwa na muda mrefu wa maandalizi kwa ajili ya kikosi chetu ndio maana imekuwa rahisi kufungwa licha ya makosa ya kiufundi ambayo tumeyafanya.
"Kwa sasa tutayafanyia kazi makosa ambayo tumeyafanya kwa ajili ya kufanya vizuri mechi zetu za ligi kwani tuna mchezo dhidi ya Mwadui FC, nina amini utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana," amesema.
Sababu siyo za kiufundi ila kujitetea. Kama hamkuwa na maandalizi uliingiza timu ya nini?
ReplyDeleteTufanye KMC wao walikuwa na maandalizi ya kutosha maana Corona wao haikuwahusu? Kocha sababu hazina mshiko.
ReplyDeleteSababu ni kuwa mpo dhaifu na Hakuna jengine
ReplyDeleteMbona hawa waandishi hawaendi kuwahoji wachezaji wa Simba mara kwa mara mmeligundua hili??? Je ni kweli kuwa, Wanatumika kuidhoofisha Yanga hapa nyie hamjajiuliza kwanini waandishi na vyombo vya habari vya mtaani vinapata access kirahisi ya kufikia wachezaji wa klabu ya Yanga na kuwaingilia kwenye maisha yao ya kila siku kwa vigezo vya kutafuta habari?...simaanishi wasihojiwe ila kuna urahisi mno kuwafikia professional wa Yanga kuliko wa Azam au Simba....
ReplyDeleteSasa sio wote wanania nia nzuri wanapoenda kuwahoji wachezaji kuwepo na mipaka ya kuwafikia wachezaji maadui wanatumia mianya hii kupenyeza "fitina" tafadhali Uongozi wa Yanga mlifikirie hili timu inazungukwa na wafitini, maadui waliovaa ngozi ya kondoo na wanafiki wenye lengo moja tu kuidhoofisha Timu ya Yanga.
Exposure imekuwa kubwa sana ya Wachezaji wenu kwenye media za mitaani....kwa kigezo cha kutafuta habari waandishi wanaweza wakatumiwa na maadui....umakini unatakiwa sana
Ahsanteni Wenu Katika Maoni!
Daima Mbele Nyuma Mwiko!
Twenzetu kwenye Mabadiliko!