July 1, 2020


INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ametoroka kambini jana wakati wachezaji walipokuwa wakijiaandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar.

Kwenye mchezo huo Morrison hakuwa sehemu ya mchezo ambapo Yanga iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na uongozi wa Yanga kwa sasa ambapo ishu kubwa inaeelezwa kuwa ni kuhusu mkataba wake ambao kila mmoja anasema jambo lake.

Uongozi wa Yanga unasema kuwa Morrison ana kandarasi ya miaka miwili huku mchezaji mwenyewe akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita ambao unameguka msimu utakapoisha.

Habari zinaeleza kuwa wakati wachezaji wakiwa kambini huku ulinzi ukiwa ni mkali Morrison alimua kusepa na alipobanwa aliwazidi ujanja walinzi na kusepa zake kuendelea na mipango yake mingine.

 Morrison ametupia jumla ya mabao matatu na ana pasi tatu ndani ya ligi huku kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia bao moja.

4 COMMENTS:

  1. Msimlazimishe kama hakutakini nynyi mmeshafanikiwa kusajili wachezaji wa kigeni zaidi ya 30 na mna uwezo wa kusajili zaidi ya hao tena bora kuliko Morrison

    ReplyDelete
  2. Unaweza kumpeleka punda hadi kisimani ila huwezi kumlazimisha kunywa maji

    ReplyDelete
  3. mgomo baridi huo,yanga mmwachie ashawapa ujumbe wa vitendo

    ReplyDelete
  4. Hata Tshishimbi walisema ameshaini mkataba mpya na picha ya video ikarushwa kwebye mitandao. Juzrikati hao hao wakasema hajasaini mkataba mpya bali wapo kwenye mazungumzo. Tshishimbi hajacheza tangu ligi irejee baada ya likizo ya covid-19

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic