July 1, 2020


KIUNGO wa Klabu ya Kagera Sugar, Awesu Awesu amesema kuwa hajui sababu ya kupewa kadi ya pili ya njano iliyomfanya atolewe nje jumla kwenye mchezo huo kwa kadi nyekundu.

Yanga jana iliikaribiisha Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali ambapo Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Bao pekee la Kagera Sugar lilifungwa na Awesu Awesu dakika ya 19 huku yale ya yanga yakijazwa kimiani na David Molinga dakika ya 52 na lille la ushindi likipachikwa kimiani na Deus Kaseke kwa mkwaju wa penalti.

Awesu alionyeshwa kadi mbili za njano jambo lililofanya aonyeshhwe kadi nyekundu na mwamuzi wa kati jambo ambalo amesema kuwa hatambui sababu ya yeye kuonyeshwa kadi hizo.

Awesu amesema:"Sikuongea jambo lolote kadi ya kwanza nikishangaa namna nilivyopewa nikasema sawa, kadi ya pili nilikuwa nimechezewa faulo nikawa namtoa mchezaji mwenzangu maana nilishajua amepanic nashangaa nakutana na kadi nyingine sijui ilikuaje, sijaongea jambo lolote na wala sijatukana aulizwe hata refa mwenyewe.

"Niliyatarajia kwa kuwa tunacheza na timu kubwa na kongwe ambazo zina maagizo, hivyo kufungwa sijashangaa ni jambo la kawaida, ninachoumia ni kwamba nimeigharimu timu na bado tuna mechi za kucheza".

Msimu uliopita wa mwaka 2019, Kagera Sugar ilikwamia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na msimu huu imekwamia pia hatua ya robo fainali.


11 COMMENTS:

  1. Wanaoibeba yanga ifike mahali waone hata aibu basi

    ReplyDelete
  2. Mnaonunua mechi pia muone aibu basi

    ReplyDelete
  3. Hivi nyie Mikia ni mashabiki wa timu ngapi? Mara Namungo, Ndanda, Kagera Sugar... mtaumia sana. Kagera wenyewe wapo kimyaa!

    ReplyDelete
  4. Kwani kwa maamuzi yale kwa nini tusiamini kuwa yanga ananunua mechi kupitia marefa na bodi ya ligi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa Yanga alinunua hata mechi na Simba 08/03/2020

      Delete
  5. Kocha wa Kagera kashindwa hata kuzungumza.Lililotokea hata kwa mimi mpenzi wa Yanga ni aibu. Napenda timu yangu ishinde lakini sio kwa uamuzi wa kijinga uwanjani. Tunasema Simba wamebebwa lakini level ya jana ta uamuzi haitusaidii kwenye madai yetu.Kagera walistahili penalti baada ya mchezaji wao kuangushwa na Mnata.Penalti yetu faulo ilifanyika nje ya box.
    Mchezaji wa Kagera alipewa kadi ya pili ya njano huku yeye ndio kafanyiwa faulo.Sijawahi kutetea ubebwaji hata kwa timu yangu.Lililotokea jana uwanjani ni kashfa.

    ReplyDelete
  6. We kwel si mzalendo wa timu yako...penalt ipi wslokataliwa kagera....na je ya fei toto mbona huisemi acha mamno yako hayo kuskiliza mikia na we ukawafatisha

    ReplyDelete
  7. Uzalendo ni kusema uongo?Mimi sijali mikia wanasema nini!Unaweza kudai kwamba Metacha hakumfanyia mchezaji wa Kagera faulo? Rudia kuangalia marudio!Sidhani kwamba unapenda Yanga ibebwe!Tunawalaumu mikia kwa kubebwa tukibebwa sisi tunashangilia tukidai kwamba ni uzalendo.Huwezi kuhubiri watu wanywe maji huku wewe unakunywa mvinyo.Unapoteza moral authority kukemea ubebwaji wakati ikihusu timu yako unatetea kwa kisingizio muflis cha uzalendo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Achana naye huyu si mwananchi. Ni Mkia

      Delete
  8. Tabu mimi sio shabiki fuata upepo. Najua miiko ya kusema kweli na role model wangu katika wanachama wa Yanga ni Barnabas Maro.Inawezekana hata humjui. Sio Yanga fuata upepo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic