IHEFU wana balaa ndani ya Ligi Daraja la Kwanza baada ya kupanda kibabe kucheza play off na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka ndani ya Ligi Daraja la Kwanza kupanda kupitia playoffs tangu mfumo huu uanze.
Ilimaliza Ligi Daraja la Kwanza ikiwa nafasi ya pili iligongana pointi na Dodoma FC ambayo ilipanda Ligi Kuu jumlajumla zote zikiwa na pointi 51 tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.
Ihefu walifunga mabao 33 huku Dodoma FC ikifunga mabao 38.
Ilianza kwa kuangukia pua mchezo wa kwanza wa Play Offs dhidi ya Trans Camp uliopigwa Uwanja wa Uhuru Julai 17 majira ya saa 10:00 jioni kwa kuchapwa mabao 3-0.
Wafungaji kwa upande wa Trans Camp walikuwa ni Nisije Mwambungu dakika ya 56,Prosper Pius dakika 78 na Hussein Saleh dakika ya 85. Ngoma ilipinduliwa pale Mbeya, Julai 22 Uwanja wa Highland Estate kwa Ihefu kuibuka washindi wa mabao 3-0 ambapo mabao yalipachikwa na Sudi Mlindwa dakika ya 21,Joseph Kinyozi dakika ya 78 na Mussa Lussewa dakika ya 89.
Matokeo hayo yalifanya mshindi atafutwe kwa penalti kwa kuwa ngoma ilikuwa ni 3-3 na Ihefu ilishinda kwa penalti 4-2.
Ikaanza na Mbao sasa ambao waliponea chupuchupu kushuka daraja jumla, Julai 29 Uwanja wa Highland Estate na kushinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza.
Dakika ya tatu Steven Mwaijala alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti na bao la pili lilipachikwa na Mlindi Tangai dakika ya 83 na kuwafanya wawe mbele kwa mabao 2-0.
Mchezo wa pili na wa mwisho ulichezwa jana, Agosti Mosi, Uwanja wa Kirumba ambapo Mbao ilishinda kwa mabao 4-2 na kutolewa kwa faida ya mabao ya ugenini ambayo Ihefu waliyapata.
Mabao ya Mbao yalifungwa naWazir Junior dakika ya 07 na 45+1, Michael Masinda alijifunga dakika ya 45+2 Datus Peter dakika 90+3 kwa penalti.
Yale ya Ihefu yalifungwa na Joseph Kinyozi dakika ya 41 na Willy Mgaya alifunga bao la ushindi dakika ya 88.
0 COMMENTS:
Post a Comment