BAADA ya Simba kumtangaza Bernard Morrison kuibukia ndani ya kikosi cha Simba akitokea Yanga, tayari jambo jingine limeibuka baada ya Shirikisho la soka Tanzania, (TFF) kuwaita Yanga kesho makao makuu kuhusu suala hilo.
Morrison yupo kwenye mvutano mkubwa na Yanga hasa kwenye suala la mkataba ambapo yeye alisema kuwa mkataba wake ulikuwa wa miezi sita huku Yanga wakisema kuwa ana dili la miaka miwili.
Jana, Agosti 8, Simba ilimtambulisha Morrison ndani ya Simba jambo ambalo limevuta mvutano ambapo Yanga ilitoa taarifa kwamba inalifuatilia suala hilo ili kuweza kuchukua hatua.
Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa kesho TFF itatoa hukumu ya kesi ambayo ilifunguliwa na Yanga kuhusu mkataba wa Morrison wa miaka miwili na hatma yake kuibukia Simba itajulikana.
"Bado sakata la Morrison halijaisha kwani kuna ile kesi yake kuhusu suala la mkataba hivyo kesho mambo yote yatakuwa hadharani, mbivu na mbichi zitajulikana," ilieleza taarifa hiyo.
Morrison amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo uwezo wake wa kucheza mpira ndani ya uwanja pamoja na kuuchezea mpira viliifanya Simba ikakubali uwezo wake.
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara hivi karibuni alisema kuwa miongoni mwa wachezaji wanaojua kulazimisha kuingia ndani ya box ni pamoja na Morrison.
Kesi ilifunguliwa na Morrison. Akidai kwamba hana mkataba. Yanga hawafungua kesi kama unavyodai.Yanga ndio walalamikiwa kwenye hoyo kesi. Mlalamikaji ni Morrison.
ReplyDeleteKesi ilifunguliwa na Yanga mkubwa
DeleteAliyeanza kushitaki ni Morison na siyo yanga yanga walifunhua kesi baadae kabisa na hukumu ya kesho inahusu kesi waliyofungua yanga
DeleteAnachosema jamaa ni kweli kesi imefunguliwa na Morison sio Yanga
DeleteWewe unafurahia tu mchezaji kusajiliwa kwenye timu yako mambo mengine hufuatilii, sasa subiri timu yako nayo ijibu mashitaka juu ya hili. Kiongozi anayejitambua anayetaka mambo yafanyike kiueledi na si kimihemko kama akina Manara amejiuzulu kuashiria kwamba hapa kuna shida, upo?
DeleteKwel nyie mashabiki wa yanga mmeshachanganyikiwa tayar
ReplyDeleteAliyefungua kesi ya mkataba ni Morrison. Kesi ya Simba kuongea na Simba ndio imefunguliwa na Yanga kama ya Mwalebela na Chama iliyofunguliwa na Simba. Mimi ni Yanga lakini unaona hata reaction ya Engineer Hersi sio serious.Isije ikawa walifikia makubaliano kwamba ata sain kama Tshimbishimbi lakini hakuna mkataba wa kisheria.
ReplyDeleteMorrison kuongea na Simba. Sahihisho hapo juu.
ReplyDeleteMashabiki wa Simba mnapanick nn? Wenye kujielewa na kuona madudu yenu ndani ya timu yenu wameshaanza kujiuzulu. Na bado. Tutachukua hatua stahiki na za mfano.. Tulieni. Ni suala la muda tuu mbivu na mbichi zitakuwa wazi
ReplyDeleteWe unachekesha kweli Morrison kama angekuwa na mkataba halali na Yanga kulikuwa kuna haja gani ya T.F.F kuchelewesha kutoa uamuzi juu ya suala hilo yani mkataba upo wa kihalali sasa kuna kigugumizi kina toka wapi cha kusema ana mkataba na Yanga mlivyokuwa mawazo yenu kama manyani mnafikiri senzo anaondoka Simba kwa sababu ya ishu ya morrison, hamjiulizi Tshishimbi mliambiwa kasaini miaka miwili na picha mkaonyeshwa leo yupo wapi tutaona kesho ukweli utajulikana
Delete