September 15, 2020


MSIMU wa 2020/21 wa Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga itarushwa moja kwa moja ndani ya chaneli ya  Azam TV.


Leo Septemba 15 umefanyika uzinduzi rasmi kwa ajili ya kuanza kurusha matangazo hayo ndani ya studi za Azam TV.

 Ligi hiyo ya Ujerumani itaonyeshwa katika kiwango cha HD kwa lugha ya Kiswahili kupitia kifurushi cha shilingi 18,000. Ligi hiyo inaanza Septemba 18, 2020.

Sasha Nella, Meneja wa Michezo wa Azam Media amesema kuwa:- “Hatutakuwa na La Liga, lakini tumeongeza nguvu kwenye Ligi Kuu Bara, (VPL) ili nayo ifikie viwango vya Bundesliga." 

Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imeanza kutimua vumbi Septemba 6 kwa sasa imeshakamilisha mzunguko wa pili na mechi zote 18 zimerushwa live ndani ya Azam TV.

3 COMMENTS:

  1. Azam mnazingua badala ya kuonyesha laliga mnaipiga chini laliga mnaileta bundasliga

    ReplyDelete
  2. Kweli mnazinguwa mngeweka zote channel tofauti watu waone kila 1 atavutiwa ile anapenda

    ReplyDelete
  3. Ligi gan munatuletea yan haina hata mvuto

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic