UNAAMBIWA
usajili una sarakasi nyingi kuliko zile ambazo wakati mwingine unakutana nazo
ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo imeanza kutimua vumbi Septemba 6..
Timu nyingi
zilikuwa zinapambana kupata saini za wachezaji zipo ambazo ziliishia kuwaona
wakitambulishwa kwingine na zipo ambazo ziliwakosa wachezaji wao kwenye timu
zao.
Cheki namna sarakasi za usajili zilivyokuwa ndani ya Bongo, kwenye dirisha lililofunguliwa Agosti Mosi na kufungwa Agosti 31 namna hii:-
Paul Nonga
Mhambuliaji
mpya wa Gwambina FC yenye maskani yake Mwanza,itashiriki Ligi Kuu Bara msimu
wake wa kwanza baada ya kufanikiwa kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.
Vita yao ya
kuwania saini ya Nonga ilikuwa dhidi ya Namungo FC ambao walimtumia nyota huyo
nauli mwanzoni kabisa mwa mwezi Agosti ila aliwachunia kwa kuwa alikuwa ana
dili tano mkononi akivuta picha wapi dau litakuwa kubwa.
Gwambina
walipomfuata kabla hata wiki haijaisha alikubali kumwaga wino na kuamua
kuwarudishia Namungo FC nauli ambayo ilikuwa ni laki moja.Kaibukia Gwambina
akiwa mchezaji huru ambaye alikuwa anakipiga Lipuli FC na alifunga mabao 11.
Ibrahim Ame
Agosti 5
alimalizana na Simba, ila Agosti 4 inaelezwa kuwa aliletwa Dar na mabosi wa
Yanga ili waongeze nguvu ndani ya kikosi chao kwa kuziunganisha pacha zile
mbili kutoka Coastal Union.
Mchezo waliocheza Simba ni kusepa na Ame mpaka Kibaha, kisha wakarudi naye na kumpeleka Posta ambapo walimalizana naye kwa kumpa dili la miaka miwili, Yanga wakabaki kuwa mashuhuda wa pacha wa Bakari Mwamnyeto akiwa ndani ya Simba alipotambulishwa rasmi Agosti 16.
Bakari Mwamnyeto
Mzawa
aliyesajiliwa kwa dau matata, Mwamnyeto ni namba moja. Inaelezwa kuwa Yanga
walivunja benki kwa kutoa milioni 170 ili kumpata beki huyu chipukizi.
Simba
walianza hesabu kitambo kuipata saini ya beki huyo. Habari zinaeleza kuwa
gharama nyingi za awali zilikuwa zinatolewa na mabosi wa Simba, hawakuwa na
chaguo waliposhtuka anaibukia Yanga, Agosti Mosi.
Bernard Morrison
Jamaa huyu
msumbufu kinoma mpaka mwenyekiti wa Kamati ya Hadhi ya Wachezaji Tanzania,
Elias Mwanjala aliweka wazi kuwa amewapa usumbufu mkubwa hasa kwa kesi yake
kuhusu mkataba wake ndani ya Yanga.
Yanga
ilikuwa inasema kwamba, ana mkataba wa miaka mwili huku mchezaji akisema kuwa
ana mkataba wa miezi sita na umekwisha, kumwaga kwake wino Simba kuliongeza
utata na kufanya mambo yawe makubwa.
Kesi ya
shauri lake iliinguruma kwa muda wa siku tatu, kuanzia Agosti 10 mpaka Agosti
12 ilipotolewa hukumu ilieleza kuwa mkataba ulikuwa na mapungufu na kumfanya
Morrison kushinda na kuwa ni mchezaji huru, ila kwa sasa ana kesi ya kujibu kwa
nini alisaini dili Agosti 8 ndani ya Simba ilihali alikuwa ana kesi ya
kimkataba.Kesi yake imepelekwa Kamati ya Maadili ya Wachezaji.
Awesu Awesu
Kiungo huyu
mwenye rasta rekodi zinaeleza kuwa amefunga jumla ya mabao saba, sita ndani ya
ligi na moja kombe la Shirikisho aliwatungua Yanga, Uwanja wa Mkapa.
Yanga
walikuwa na mpango wa kuipata saini yake na mchezaji alikubali kutua, kabla hawajamalizana
naye, mabosi wa Azam FC waliibuka naye na kumtangaza ndani ya kikosi chake kwa
kumpa dili la miaka miwili Julai 30, Yanga wakamaliza hasira kwa kuinasa saini
ya Zawadi Mauya na kumtambulisha Julai 31.
Ally Niyonzima
Bado Azam
waliwazidi ujanja tena Yanga kwa kuwapoteza mbele ya Niyonzima ambaye alikuwa
amekubali kutua Yanga.
Akiwa zake
Rwanda, mabosi wa Azam wakamfungia safari na kumshusha Dar fasta na kumpa dili
la miaka miwili,Agosti Mosi akavishwa jezi ya Azam FC na tayari yupo zake
Chamazi kwa sasa.
Wazir Junior
Hapa sasa
Yanga walicheza kinoma kwa kuwapoteza mazima Azam FC.Hesabu za Azam zilikuwa
kuinasa pia saini ya mchezaji wao wa zamani, Waziri akiwa kwenye majukumu yake
ya mbele ya Ihefu FC, Agosti Mosi, tayari Azam FC walikuwa ndani ya uwanja na
Yanga pia.
Hapa machale
kwa Yanga yalianza mapema na kuamua kumshtua kiongozi mmoja wa Mbao ambaye
alimbeba mchezaji mpaka chooni, huko alitoa jezi na kutupia viwalo vingine
akatoka kininja na kupelekwa hotelini, Azam walisubiri mpaka wakasubiri ngoma
ikawa nzito.Wanakuja kushtuka Agosti 2, nyota huyo mwenye mabao 13
anatambulishwa ndani ya Yanga.
Duuuh noma sana
ReplyDelete