September 12, 2020



MENEJA wa Klabu ya Tottenham, Jose Mourinho amewapiga mkwara wachezaji anaowataka kuwapa dili ndani ya timu hiyo kwa kusema kuwa ikiwa wanahofia kushindana na mshambuliaji wake namba moja Harry Kane na Son Heeung-min hawezi kufanya nao kazi.

Mourinho ambaye huwa haishiwi maneno inaelezwa kuwa  klabu yake ipo kwenye hesabu za kupata saini ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Patson Daka inaelezwa kuwa amepunguza ile shauku ya kutaka kujiunga na timu hiyo.

Licha ya kwamaba Tottenham inahitaji kufanya usajili bado ipo kwenye mchakato wa kujua ni yupi atakuwa sahihi kutua ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Ripoti zinaeleza kuwa Mourinho amesema kwamba akiwa kwenye mpango wa kuwatafuta washambuliaji wapya hana kazi ya kuwashawishi yeye zaidi wao wanapaswa wamshawishi yeye ili awape mkataba na ikiwa mshambuliaji ana hofu ya kujiunga na timu yake kisa anahofia ushindani huyo hawezi kumfaa kabisa.

"Ndio ninahitaji mshambuliaji hilo lipo wazi, ila kama hataki kuja ndani ya kikosi kwa kuwa nina Harry Kane, Son, Lamela, Lucas Moura unadhani nini kitafuata basi nitamwambia kwaheri.

 "Hata timu yenyewe inajua kwamba ninahitaji mshambuliaji ila sio katika hali hii," amesema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic