September 11, 2020

 


KAGERA Sugar, inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime leo Septemba 11 imelazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Gwambina, Mwanza.


Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kupambana kusaka pointi tatu muhimu ila mpaka dakika 90 zinakamilika wamegawana pointi mojamoja.


Timu hizi mbili zimekuwa na matokeo yanayofanana kwa kuwa kwenye mechi za ufunguzi wa ligi walipata matokeo yanayofanana viwanja viwili tofauti.


Gwambina ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Biashara United Uwanja wa Karume na Kagera Sugar ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania,  Uwanja wa Kaitaba. 


Kagera Sugar inarejea Kaitaba kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Septemba 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic