September 16, 2020



KIKOSI cha Yanga, leo Septemba 16 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Mlandege FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Yanga ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa nyota mpya wa kikosi hicho, Wazir Junior aliyeibukia kikosini humo akitokea Klabu ya Mbao. 

Amepachika bao hilo dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti baada ya mpira uliopigwa ndani ya box na Haruna Niyonzima mwamuzi kutafsri kuwa mchezaji wa Mlandege aliunawa.


Kipindi cha pili Yanga ilibadili kikosi upya na kuanza mashambulizi kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani zaidi kipindi cha kwanza kuliko kile cha pili.

Bao la pili lilipatikana dakika ya 59, kupitia kwa Tunombe Mukoko na kuwafanya Mlandege FC kupoteana ndani ya uwanja.

Dakika ya 75 mchezaji wa Mlandege Ibrahim Juma alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa awali kadi ya njano ilikuwa dakika ya nne.

Baada ya mchezo huo Yanga inaanza hesabu za kuifuata Kagera Sugar kwa ajili ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Septemba 19.

5 COMMENTS:

  1. Aina gan ya uandish unaotumia. Kama unaiga stail ya fotmob kuna mahal unachemka. Uandsh huo ungekuwa mzur kama unapost knachoendelea live na sio mchezo ushaisha

    ReplyDelete
  2. Naona juu anaandika FT 1-0 ndani anaandika Yanga 2 Mlandege 0,fukezeni hao waandishi feki muweke waandishi wanaojielewa.

    ReplyDelete
  3. Bora post ifutwe tu, maana kwa uandishi huo, hata Mtoto wa darasa la Sana ansyejifundisha uandishi wa habari hawezi kuandika hivyo

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Waandishi mjitahidi kuandika vizuri hatuwaelewi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic