September 16, 2020

 


LEO Septemba 16, kikosi cha Yanga kinachonolewa na Zlatko Krmpotic raia wa Serbia kitashuka Uwanja wa Azam Complex kumenyana na Mlandenge FC ya kutoka visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki.


Mchezo huo utapigwa saa 1:00 usiku  una malengo ya kuboresha viwango vya nyota wa Yanga kutokana na kukosa mechi fitness baada ya kutokuwa na muda mrefu wa pre-season kutokana na janga la Virusi vya Corona. 


Yanga ilianza maandalizi ya msimu wa Ligi Kuu Bara Agosti 15 ikiwa na wachezaji11, ambapo ilianza kufanyia mazoezi yake Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam ila kwa sasa imeweka kambi jumla Kigamboni. 


Tayari imeshacheza mechi mbili ndani ya ligi na imeshinda moja mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0 na kuambulia sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons zote Uwanja wa Mkapa. 


Mechi yake inayofuata ni dhidi ya Kagera Sugar,  Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

8 COMMENTS:

  1. Mnakumbuka shuka kumekucha, kweli ninyi mikia a.k.a utopolo wenzenu washapita hko ninyi ndo kwanza mnaanza

    ReplyDelete
  2. Sasa ww kinacho kuuma nn ynga yetu cc na uzur alie wahi kambi na aliye chelewa matokeo yaleyale kwn mnapoint ngap? Tim ya kocha kishingo

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😆😆😆 utopolooo mnafurahisha kweli, kababu kenu muda si mrefu mtakatimua

      Delete
  3. Replies
    1. 😆😆😆 kweli wanapiga mabonanza yakidizaini wapate hela ya nauli Hawa utopolo

      Delete
  4. Hawajielewi hao Manyani fc wanavyomsifia Carlinhos kama hujawahi kumuona akicheza unaweza kusema ni mchezaji hatari kumbe punga tu, alafu huyo Kisinda sijui yani hajafikia hata nusu tu ya uwezo wa mtu kama OKWI tarehe 18 wanavunja tena timu na wanasajili tena upya, yani mpaka wavunje timu mara 20 ndipo wanaweza kuja kuchukua ubingwa ila sasa hv ni utopolo mtupu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanachama wengne bwna cjui hawna akil xaxa okwi nmchezaji wawap? Njoo jangwan 2kupe elimu ukawafndishe na wengne walio kama wewe

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic