September 11, 2020

 



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa  Septemba 13, Uwanja wa Mkapa.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Septemba 6, Uwanja wa Mkapa.

Mbeya City wao wataingia uwanjani wakiwa wametoka kupoteza kwa kufungwa mabao 4-0 mbele ya KMC, Uwanja wa Uhuru. 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote zilizo mbele yao hivyo watapambana kupata pointi tatu.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa msimu uliopita wa 2019/20 timu zote mbili zilitoshana nguvu kwenye mechi zao zote mbili walizokutana ndani ya uwanja.

Ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ngoma ilikamilika kwa sare ya bila kufungana na ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa ulikamilika kwa kufungana bao 1-1.

4 COMMENTS:

  1. Haina haja ya kuifanyia hesabu na kuyakuza mnakwenda kucheza na timu dhaifu ambayo hivi Juzi ilichapwa mabao mane kwa bila na timu chipukizi KMC

    ReplyDelete
  2. 😆😆😆 utopolo wanajikweza kwa team mfu wakishinda wajione wanaweza, wakati mbeya city IPO dhohofu kiafya yankimichezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ihefu ni timu iliyowalaza na viatu licha ya uchanga wake katika ligi kuu. Unapofanya ulinganifu, tumia vigezo halisi na si vya kukariri

      Delete
  3. Gongowazi ndio hawakuona kuwa aliyelaza ni yule aliyepata goli mbili na aliyelazwa ni yule aliyepata goli moja au ndio hawayajuwi hayo? wao wanaona aliyelazwa ni yule Aliyeondoka na kamili na pointi tatu. Kweli akili zinawaruka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic