UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kushinda mechi zote zilizobaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ili kutimiza lengo lao namba moja la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Azam FC imecheza mechi sita ndani ya ligi ambazo ni dakika 540 imeshinda zote, imefunga mabao 12 na kufungwa mabao mawili na pointi zake kibindoni ni 18.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa hesabu kubwa za timu kwa sasa ni kuona inamaliza mechi zake zote bila kupoteza.
“Tuna kikosi kipana na imara na kila mchezaji anaonyesha juhudi zake ndani ya uwanja. Kilichopo ndani ya timu ni kuona namna gani tunaweza kushinda mechi zetu zote zilizopo mbele yetu na hilo linawezekana.
“Msimu uliopita tulianza vizuri ila baadaye tuliteleza hasa kwa upande wa safu ya ushambuliaji hilo tumelifanyia kazi na kwasasa tupo imara, kikubwa mashabiki watupe sapoti,lengo letu ni kuona kwamba tunaweza kutwaa ubingwa,” amesema Amin.
Oktoba 20, Azam FC ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu FC kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Sokoine saa 8:00 mchana.
Mchezo wake wa sita ilicheza na Mwadui FC Uwanja wa Azam Complex na ilishinda mabao 3-0 na kuifanya ifikishe pointi 18 ikiwa nafasi ya kwanza.
Chanzo:Championi
Mtashinda hiyo ihefu ni uchochoro tu hamna timu hapo zaidi ya maneno ya watu wa rujewa ndio yamejaa tena wafungeni 10
ReplyDelete