October 18, 2020

 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Cedric Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye ubora kwa rekodi za mechi zao za mwisho.


Yanga ambao ni wenyeji walishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, Oktoba 3 ambapo ulikuwa ni mchezo wa mwisho kwa Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi jumlajumla.


Polisi Tanzania wenyewe walishinda bao 1-0 dhidi ya KMC, Oktoba 5 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Baadhi ya picha za mazoezi ya Yanga wanayofanyia Kigamboni hizi hapa:-




Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi tano. 

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic