October 21, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons kesho sio mwepesi kutokana na uimara wa wapinzani wao hao ambao kwa sasa wanatumia Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Prisons kesho, ikiwa ni mchezo wao wa sita ndani ya ligi.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa sio kazi nyepesi kupata ushindi mbele ya Tanzania Prisons kutokana na uimara wa kikosi hicho.

“Mchezo wetu wa Oktoba 22 dhidi ya Tanzania Prisons sio mwepesi kwani tunakutana na timu ngumu na yenye wachezaji wapambanaji muda wote. Unajua timu za majeshi zenyewe muda wote zipo fiti hapo unaweza kujua Simba tunakwenda kukutana na timu ya aina gani.

“Kwa kuwa sisi ni mabingwa watetezi basi lazima tuingie kibingwa na tucheze tukiwa ni mabingwa watetezi, mashabiki wetu watupe sapoti ili timu ipate matokeo kwani tunahitai ushindi,” amesema.


Kwenye mchezo wa nyota Chris Mugalu anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji baada ya mshambuliaji namba moja Meddie Kagere mwenye mabao manne kusumbuliwa na majeraha.


Pia nahodha, John Bocco ambaye ni mzawa wa kwanza kufunga mabao zaidi ya 100 ndani ya ligi kwa sasa naye anasumbuliwa na majeraha.


Mchezo wa mwisho Simba kwenye ligi ilicheza dhidi ya JKT Tanzania na iliweza kushinda kwa mabao 3-0 inakutana na Prisons ambayo imetoka kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania.

6 COMMENTS:

  1. Kama huna cha kuandika acha presha ipi wanao wapa mabingwa? Acha unafiki.na kesho usiandike watakavyo fungwa hao unawo wasifia?

    ReplyDelete
  2. Hahahahaaaa..... Mnatesekaeeee.....kesho tunapga mtu 3:0.... Mugalu 2

    ReplyDelete
  3. Hahahah mikia fc bwana lazima mkae 2-1.

    ReplyDelete
  4. kweli mara zote game dhidi ya prison ni ngumu but hope tutashinda biidhinillah

    ReplyDelete
  5. Umeongea kimichezo sana....huwezi kupambana na adui usiyemjua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic