October 21, 2020


 PRINCE Dube, kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara amesema kuwa kwa sasa hana hesabu na tuzo ya kiatu cha ufungaji bora kwa kuwa kitamtoa kwenye ramani ya kupambania timu yake ya Azam FC kufikia malengo ya kuweza kutwaa ubingwa.


Tuzo ya kiatu bora ambayo Dube ameipotezea ipo mikononi mwa Meddie Kagere mshambuliaji namba moja wa Simba ambaye alitwaa msimu uliopita baada ya kufunga mabao 22. 


Kwa sasa Azam FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi saba na kushinda zote kibindoni ikiwa na pointi 21. Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 14 na kinara ni Dube mwenye mabao sita.


Pia Dube amehusika kwenye mabao 10 ndani ya Klabu ya Azam FC kwa kuwa mbali na kufunga mabao sita ametengeneza jumla ya pasi nne ambazo zilileta mabao.


Jana, Oktoba 20 wakati Azam FC ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine pasi zote za mabao alikuwa mpishi na kufanikisha rekodi ya timu yake kushinda mechi saba mfululizo.

Dube amesema:-"jambo la kwanza ni kuona timu inashinda kisha suala la mimi kufunga litafuata baadaye ila sio kwa sasa siwezi kufikiria kuhusu kufunga na kufikiria tuzo ya ufungaji bora.


"Kitu cha kwanza kwangu mimi na wachezaji wenzagu ni ushindi kisha suala la nani atafunga iwe mimi ama mwingine ni sawa, lakini tunafurahia kwanza ushindi," amesema. 

Dube ana tuzo ya mchezaji bora ya mwezi Septemba. vita yake kwenye kiatu cha ufungaji bora ni dhidi ya Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao manne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic