October 19, 2020

 


KIKOSI cha Simba leo Oktoba 19 kimeanza safari kuelekea Mbeya ambapo kitakaa kwa muda wa siku mbili kabla ya kuelekea Rukwa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons. 

Mchezo huo wa raundi ya sita utachezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela,  saa 10:00.

Leo wapinzani wao Tanzania Prisons watakuwa kibaruani Uwanja wa Jamhuri Dodoma kumenyana na JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara wakimaliza mchezo huo watarejea Rukwa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba.


Kwa sasa Simba ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi zao ni 13 baada ya kucheza mechi tano na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 14.


Prisons ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tano na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao matatu.

7 COMMENTS:

  1. kuwachezesha leo Prison kule Dodoma kisha unawarudisha Rukwa kwa Bus kucheza na simba baada ya siku tatu ni wazi hapo mnawachokesha wachezaji na kuipa urahisi Simba kushinda mechi hiyo ya alkhamis !!! kuna swali la kujiuliza hapo katika upangaji wa hizi mechi !!

    ReplyDelete
  2. Sijaona Sababu Ya Simba Kuto Kucheza Mechi Ya Vpl Mda Wote Huo Wanataka Simba Ipowe Tuna hamu Ya Na Mech Za Back To Back

    ReplyDelete
  3. Mikia fc manabebwa sana ila kifo chenu kipo tu pale pale

    ReplyDelete
  4. Kwani nyinyi kila simba inapo cheza kinawauma mini? Nyinyi kandambili za chooni? Si mmeleta kocha kwa bwembwe kama yy ni mchezaji mtamfukuza huyo tarehe 7

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaan We Subiri Tuone Maana Si Kwa Tambo Hizo Mimi Na Subiri Tar 7 Tufanye Yale Tuliyo Wafanyia Nusu Fainal Ya AFA Wanyamaze

      Delete
  5. Bado tutaendelea kupiga kelele ratiba kuna timu zinabebwa tff jitathimini

    ReplyDelete
  6. Kila mmoja acheze mechi zake.Yanga maneno mengi.Timu yenu bado sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic