October 21, 2020

 


KIKOSI cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00.


Utakuwa ni mchezo wa Kwanza kwa Yanga chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili kukinoa kikosi hicho.


Kaze anachukua mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi Oktoba 3 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na mwendo mzuri ndani ya kikosi cha Yanga. 


Mpaka anasepa, Yanga ilikuwa imecheza mechi tano na ilishinda nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mkapa. 


Ipo nafasi ya tatu na pointi zake 13 ndani ya Ligi Kuu Bara na kinara ni Azam FC mwenye pointi 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic