October 21, 2020


 BAADA ya kimya kutanda kwa muda mrefu, hatimaye Klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa kocha wa viungo wa timu hiyo, Msauz, Riedoh Berdien.

 

Ikumbukwe Riedoh aliondoka nchini kabla ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Coastal Union na kurejea Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja, lakini tangu alipomaliza muda wake wa mapumziko mafupi, alishindwa kurudi Tanzania kuungana na kikosi cha Yanga baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa timu hiyo.


 Riedoh amesema kuwa, amekubaliana na uongozi wa Yanga kuachana na majukumu ya kuendelea kuwa kocha wa viungo wa timu hiyo baada ya baadhi ya viongozi wa Yanga kusema kuwa hawakumpa ruhusa ya kurejea Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko.

 

Riedoh aliongeza kuwa, wakati anaondoka kwa ajili ya mapumziko, alikubaliana na Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla, Hersi Said na Kaimu Katibu Mkuu, Simon Patrick, lakini mshauri wa Yanga, Senzo Mazingisa, alikuwa hataki mtaalam huyo wa viungo arejee Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko.


“Wachezaji wengi na mashabiki walikuwa wananiambia hawataki niondoke, lakini nimefikia makubaliano na viongozi wa Yanga niondoke kwa sababu walikuwa hawataki nirudi Tanzania, kilichonishangaza ni baadhi ya viongozi kusema sikuwa nimetoa taarifa kama nitaondoka kwa ajili ya mapumziko.

 

“Wakati naondoka nilikubaliana na Mwenyekiti, Mshindo Msolla, Hersi Said na Kaimu Katibu Mkuu, Simon Patrick, lakini kumbe Senzo alikuwa hataki mimi niende Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko na kuiona familia yangu, lakini wakati naondoka yeye hakuwepo Tanzania,” alisema Riedoh Berdien.

 

Riedoh alijiunga na Yanga msimu uliomalizika, mwezi Januari, mwaka huu baada ya jina lake kupendekezwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Luc Eymael, lakini mkataba wa Riedoh na Yanga ulikuwa unatarajia kumalizika Januari, 2021.


Chanzo:Championi

8 COMMENTS:

  1. Kazi ya Senzo hiyo lengo ni kujenga utawala wake tofauti na ndo kinachoendelea kwa hiyo baada ya kufika dirisha dogo la usajili ukweli ni kwamba kwa Yanga ya Senzo mabadiliko yatakuwa makubwa sana mimi naona hata Juma mwambusi ajiandae kisaikolojia, cha msingi ni mipango na ushindi ndo vitakuwa kwetu furaha

    ReplyDelete
  2. Punguzeni kuvuruga benchi la ufundi, kuna madhara

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili pilau la benchi la ufundi linalopikwa mwisho wake litapakuliwa bokoboko

      Delete
  3. Senzo anasifiwa sasa hivi Ila baadae atachukiwa Maana timu yetu hii uswahili mwingi

    ReplyDelete
  4. Hiyo senzo anaubinfi atawavuruga hapo kweni mlijuwe hilo

    ReplyDelete
  5. Replies
    1. Nenda ukajinyonge maana naona mapov yameanza kukutoka

      Delete
    2. 😄😄😄😄 acha ukiazi wewe 👍 utopolo, bingwa wa nchi Ni Nani, bingwa anawaza kutwaa ubingwa Afrika utopolo na wenzake .bawaza Azam federation, wp na wp

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic