WAKATI Simba ikiwa imeweka makazi nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum utakaopigwa Jumatano ijayo, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa utafanya juu chini kwa kuhakikisha wanapata ushindi wa kutosha ili uwe faida kwao katika mchezo wa marudiano utakaopigwa hapa nchini.
Mchezo wa marudio, FC Platinum wataibuka Uwanja wa Mkapa ambapo inatarajiwa kuwa Januari 6.
FC Platinum anayochezea Mtanzania, Elias Maguri inatarajia kucheza na Simba katika mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo Desemba 23 katika mchezo ambao Simba itaanzia ugenini.
Ofisa Habari wa timu FC Platinum, Chido Chizondo amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa kuhakikisha wanapata matokeo makubwa katika mchezo huo kwa kuwa wanatambua ubora wa Simba inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.
"Tumejiandaa kupata matokeo mazuri, namaanisha ushindi mkubwa ambao kwetu hauwezi kuwa kikwazo katika mchezo wa marudiano, tunajua kwamba Simba ni bora lakini tutakuwa bora kwa sababu tunaanzia kwetu.
“Nadhani kikubwa ni kwamba tunaelewa Simba ni timu ya aina gani kutokana na kuweza kutumia vyanzo vyetu kufahamu baadhi ya mambo muhimu lakini tunaelewa kuna baadhi ya maofisa wao wameshaingia Zimbabwe ila hatuwezi kuhofia chochote,” amesema Chizondo.
Nyota wa 24 wa Simba wapo nchini Zimbabwe kwa sasa ikiwa ni pamoja na kiungo mkabaji chaguo namba moja kwa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, Jonas Mkude.
Mabingwa hatutaki shobo
ReplyDelete