December 20, 2020


 NYOTA mpya wa Yanga, 
Saido Ntibazonkiza ameweka rekodi yakee ndani ya ardhi ya Bongo baada ya kufunga jumla ya mabao mawili na pasi moja kwenye mechi zake mbili za mwanzo. 

Ingizo hilo jipya kwenye usajili wa dirisha dogo kutoka nchini Burundi alianza kufanya makeke kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Singida United.

Mchezo huu ulikuwa ni wa kirafiki na matokeo ilikuwa Yanga 3-0 Singida United, Uwanja wa Liti ambapo alifunga mabao mawili, moja kwa penalti.


Jana Desemba 19 kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na matokeo yakuwa Yanga 3-1 Dodoma Jiji alitupia bao moja kwa faulo na pasi moja ambayo alipiga pia kwa njia ya faulo.


Rekodi yake imekuwa ya kipekee ndani ya ardhi ya Bongo kwa msimu huu kwa wachezaji ambao wamesajiliwa dirisha dogo kwa kuwa wengi hawajaanza kuonyesha makeke ikiwa ni pamoja na Thaddeo Lwanga wa Simba ambaye anatarajiwa kuanza kufanya yake Desemba 23.


8 COMMENTS:

  1. Mmmmmh Hadi mechi za kirafk,,,,je mugalu utasemaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na Mugalu nae amesajiliwa dirisha hili dogo?

      Delete
  2. Duh, Mugalu tena amefanya kitugani chakushangaza, zaidi ya kukaa benchi, au record ya kusuguaa benchi?

    ReplyDelete
  3. Ni kweli Saido ameweka rekodi Yanga walipovheza na Singida Combine maana Singida United huwa haitokei kwenye michezo ya ligi ya daraja la kwanza

    ReplyDelete
  4. Hapa shida ni kwamba mna mtamani , Morrison kawashinda hv una akili za kutosha huyo Mgalu unayemtaja hata hata alifunga Vitalo feki na Africa Lyon sawa ,kwa Ile free Kiki standard yake kwanini usi appreciate?lkn angalizo kwenu mwaka huu Yanga hii siya Molinga,Tshishimbi,Kelvin Yondani au Yekpe mjiandae cse Kuna mido Mgabon anatua tayari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni suala la muda tu. Hata Sarpong mlimvumisha hatari. Sasa vipi kwani ana magoli mangapi striker huyo wa kimataifa? Hata mabeki tu wamemzidi uwezo wa kufumania nyavu ambayo ndilo jukumu lake ndani ya Yanga

      Delete
  5. rekodi nyingine ni kuwa ndiye babuu aliyefunga goli jana kuliko wachezaji wote waliocheza jana.Anamzidi Onyango miaka sita.na ni mzee kuliko Hamis Tambwe! Ukisikia unafiki ndiyoo huu...Aliposajiliwa Bocco na Kagere tulisikia, na hata Onyango...kumbe wanatuletea kijuza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic