KIUNGO mshambuliaji wa
klabu ya Yanga, Balama Mapinduzi amefunguka kuwa anaamini atarejea uwanjani
akiwa bora zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka kwa mara ya pili akiwa
nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa matibabu.
Balama aliyefanyiwa
upasuaji huo wa pili Januari 11 mwaka huu aliondoka nchini Desemba 3, mwaka
jana kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu, kufuatia
maendeleo yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kwanza kutoridhisha.
Balama alipata majeraha
hayo mwezi Juni mwaka jana katika mazoezi ya Yanga iliyokuwa ikijiandaa na
mchezo dhidi ya Ndanda ambapo kutokana na majeraha hayo amekuwa nje ya uwanja
kwa miezi sita na kukosa michezo 27 ya Yanga.
Akizungumzia kuhusu hali
yake Mapinduzi amesema: “Naendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka
tarehe 11, ya mwezi huu wa Januari na nashukuru Mungu upasuaji huo ulienda
vizuri.
“Nawashukuru wote ambao
mmekuwa mkinitumia salamu za pole, lakini naushukuru uongozi wa Yanga pamoja na
GSM kwa mchango wao mkubwa wa kuhakikisha narejea katika hali yangu ya kawaida,
naamini baada ya kupona nitarejea uwanjani nikiwa bora zaidi”
Mungu akuponye
ReplyDelete