January 1, 2021


 SALUM Mayanga, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa haikuwa hesabu zake kulazimisha sare mbele ya Yanga ila wachezaji wake walizidiwa mbinu mwishoni jambo lililowafanya wakaruhusu bao.


Prisons ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 52 kipindi cha pili kupitia kwa Jumanne Elifadhili liliwekwa sawa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 76.

Sare hiyo inaifanya Tanzania Prisons isepe na pointi mbili jumla kwenye mechi mbili mbele ya Yanga ambapo ule wa kwanza Uwanja wa Mkapa zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Pia mchezo wa kwanza Prisons ilianza kufunga kupitia kwa Lambart Sabiyanka na mchezo wa jana, Desemba 2020 Prisons ilianza kufunga na bao likasawazishwa.

Mayanga amesema:"Ilikuwa tunazihitaji pointi tatu kwa kuwa ilikuwa ni muhimu kwetu kushinda kwa kuwa tumepata sare basi hatuna chaguo.

"Tutajipanga kufanya vema wakati ujao kwenye mechi zetu zijazo, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti na tunawashukuru kwa kuwa pamoja nasi.

"Wachezaji pia wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana kusaka matokeo mwisho wa siku wakapata pointi moja," . 

11 COMMENTS:

  1. Kwahiyo kocha amekiri kuwa Yanga ni hatari na kiboko kwani kuzidiwa mbinu maana yake Mpinzani yuko bora kuliko wewe...Ahsante Kocha kwa kutuweka sawa!

    ReplyDelete
  2. Lazima wafurahi kiboko ya simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie mlichukia kwakuwa mlifungwa na Wajela....kiboko yenu

      Delete
  3. Haya ni wapendekezo ya saleh sio mayanga

    ReplyDelete
  4. Mlicheza jihadi, mlijua kabisa mtapigwa na yanga. Poleni sana kuikamia timu ya wananchi.

    ReplyDelete
  5. Utopolo acheni kujishaua mnadondosha mojamoja mpaka hivi sasa tayari mshadebweda mwenye nafasi yake anakuja ng'atukeni mapema tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie mlidondosha 3....Nyie mlichukia kwakuwa mlifungwa na Wajela....kiboko yenu

      Delete
    2. Mikia ikisikia inaenda kuCheza na Prisons inalia lia

      Delete
  6. Nguruwe fc hapo mlikaa dude moja

    ReplyDelete
  7. Nyie mikia si mlichomekwa kimoja mkashindwa hata kuchomoa, kwanza mseme, mara ya mwisho mliwafunga hawa wajelajela ni lini? Acheni yanga iitwe yanga, nyie SIMBA KOKO tulizeni mikia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic