January 13, 2021

 


WAKATI uliopo kwa sasa kwenye ulimwengu wa mpira ndani ya ardhi ya Bongo ni kukimbizana na masuala ya usajili kwa timu ambazo zinahitaji kuboresha vikosi vyao.

Dirisha dogo ni maalumu kwa ajili ya maboresho kwa timu mabazo zimeweza kuona kwamba zinahitaji kufanya maboresho kwenye timu zao kutokana na namna ambavyo wameona inafaa.

Awali niliweza kuweka wazi kwamba usajili wa dirisha dogo sio wa timu nzima bali ni wachezaji wachache ambao wanahitajika na benchi la ufundi kwa wakati huo ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Zipo timu ambazo zimekuwa kwenye maboresho ambapo tumeona namna ambavyo wachezaji wao walivyoweza kupata timu sehemu nyingine na wao namna walivyoweza kupata wachezaji wapya.

Maisha ya soka ni mabadiliko kila siku kwa yule ambaye anafanya vizuri anapata nafasi ya kusonga mbele na yule ambaye anafanya vibaya huwa inakuwa rahisi kuanguka na kushindwa kuendelea.

Ila kikubwa ni kwamba kwa yule mchezaji ambaye ameshindwa kupata matokeo mazuri ya kile alichokifanya na kazi ya kuweza kufanya wakati ujao.

Bado muda upo jambo la msingi ni kuweza kuweka mipango sawa katika kufanya mapambano ndani ya uwanja ili kupata kile ambacho anakihitaji.

Ninaona kwamba wapo ambao wameanza maisha mapya baada ya madili yao kujibu ndani ya uwanja na kupata timu mpya. Wengine wanapambana kurejea kwenye ubora yote ni kheri.

Jambo la msingi kwa sasa kwa wachezaji ambao wamepita timu mpya kibarua chao ni kuona kwamba wanakwenda kufanya kazi kweli.

Kwa wale ambao wapo kwenye timu zao pia bado wanajukumu la kuendelea kupambana kusaka ushindi kwa ajili ya wakati ujao.

Ukweli ni kwamba siku zimebaki chake kuelekea dirisha dogo kufungwa ambapo wale ambao wapo sokoni ikiwa watachelewa itakuwa hasara kwao.

Kwa wale ambao bado wanapambana kupata wachezaji muda wa mwisho huu hivyo wasikawie kwa kuendelea kuvuta pumzi.

Kinachotakiwa kwa sasa ile ripoti ya benchi la ufundi ifanyiwe kazi na kuwapa nafasi wale ambao wanahitajika ndani ya kikosi ili waweze kuyapata nafasi ya kufanya usajili wao.

Ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi ya Wanawake kwa msimu huu wa 2020/21 ni mkubwa na upo wazi kabisa.

Kwa zile ambazo zilishindwa kwenda na kasi hiyo zina wajibu wa kuboresha mwendo wao ndani ya ligi kwa kuboresha pale ambapo walikuwa wamekwama kwenda na kasi hiyo.

Itakuwa vizuri kwa nyakati hizi za mwisho kukamilisha mipango ya usajili na kuweza kuwapata wale wachezaji ambao walikuwa wanahitajika na timu zao.

Muda upo ila ni lala salama kwa sasa ikiwa watashindwa kukamilisha mipango yao itakuwa ngumu kurejea kwenye ushindani na kufanya kile ambacho benchi la ufundi linahitaji.

Wapo wale ambao walikamilisha mapema mpango wa usajili hawa ikiwa wamefuata mapendekezo ya benchi la ufundi ninaamini kwamba wataweza kwenda sambamba na kasi ya ushindani.

Lala salama itumike kuziweka salama timu ambazo mwendo wao ni wa kusuasua kwa kuwa hakutakuwa na muda wa kurekebisha makosa kwa msimu wa 2020/21 ikiwa timu itashuka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic