NYOTA wa kikosi cha Simba Luis Miquissone kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa jopo la madaktari akipewa huduma baada ya kupata maaumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.
Nyota huyo ameondolewa kwenye kikosi ambacho kimeweka kambi Visiwani Zanzibar na jana kiliweza kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea sehemu mbalimbali za vivutio.
Hakuwa kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Chipukizi ambacho kilishinda mabao 3-1 na kile kilichoivua ubingwa Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-0 na leo pia hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Namungo hatua ya nusu fainali.
Meneja Klabu ya Simba, Abbas Ally amesema kuwa nyota huyo yupo Dar akiwa chini ya uangalizi baada ya kushauriwa kwamba anapaswa kupata mapumziko.
"Luis yupo Dar baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum hivyo kwa sasa anaendelea na matibabu ikiwa atarejea kwenye ubora wake anaweza kuja kujiunga na timu," amesema.
Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum na imetinga hatua ya makundi ikiwa imepangwa kundi A.
Wale mapunda walitaka kumwiua kabisa. Na marefa pia wanatakiwa kuwalinda wachezaji dhidi ya uchezaji wa kibabe kama ule
ReplyDelete