January 3, 2021


 KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck imeweka rekodi ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa haijaruhusu bao la kufungwa ndani ya dakika 450 kwenye Ligi Kuu Bara.


Kikosi cha Simba kimefunga jumla ya mabao 15 katika mechi tano za mwisho ambazo ni dakika 450 za ligi msimu wa 2020/21.

Mara ya mwisho Simba kuruhusu bao ilikuwa dhidi ya Yanga Novemba 7 mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Bao la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong ambaye alimtungua Aishi Manula na bao la Simba lilifungwa na Joash Onyango ambaye alimtungua Metacha Mnata.

Pia ukuta wa Simba umeruhusu mabao matano ndani ya mechi 15 huku watani zao wa jadi Yanga wakiruhusu jumla ya mabao 7 kwenye mechi 18.

3 COMMENTS:

  1. Zile Kelele za timu ipi yenye ukuta mgumu siku hizi sizisikii

    ReplyDelete
  2. Kelele za ukuta mgumu pamoja na washambuliaji wenye mabao mengi hazipo tena

    ReplyDelete
  3. Utopolo mbio zao zinakaribia ukingoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic