January 10, 2021


IKIWA mabosi wa Yanga bado wapo kwenye hesabu za kupata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama inabidi wajipange 'kuvunja benki' kuipata saini ya nyota huyo.

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa mwamba huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/21 yupo kwenye rada za watani hao wa jadi.


Msimu wa 2019/20 alifunga mabao mawili ndani ya Simba na kutoa pasi 10 za mabao pia jina lake lilikuwa kwenye orodha ya kikosi bora  na tuzo nyingine aliyosepa nayo ni ile ya kiungo bora.

Tayari Chama ambaye mkataba wake ulikuwa unameguka msimu huu na alikuwa huru kuzungumza na timu nyingine ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Simba.

Hivyo kwa timu ambazo zimevutiwa naye ni muda wa kukaa mezani na Simba ili kujua namna gani wanaweza kuvunja mkataba.

Nyota huyo ameongeza dili la miaka mitatu kubaki ndani ya Klabu hiyo ambayo ipo chini ya Kaimu Kocha, Seleman Matola.




25 COMMENTS:

  1. Sasa mlikuwa mnawadanganya nini mashabiki wa yanga, ili iweje?

    ReplyDelete
  2. Vipi kuhusu ile nyumba ya kifahari uliyosema kajengewa kwao na Young Africans kama makubaliano yao na Chama? Kweli nimeamini ukiwa mwongo unapaswa kuwa na kumbukumbu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ha Haa huyu Jamaa Yanga Damu namanisha huyu mwandishi

      Delete
  3. Washabiki wa simba hawana akili huyo jamaaaa sio chama kama ni yeye kwanini afiche USO wake chini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa nyie ndo mna akili mliombiwa chama mchezaji wenu na mkakubali,mliombiwa mmeenda CAS Kila siku sinema mpya ama kweli utopolo itabaki kuea utopolo tu

      Delete
  4. Kama kuna mtu kajenga nyumba zambia aende akaibebe nyumba yake. Mashabiki wa yanga ndio hawana akili wamezoea kudanganywa na gsm

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unajua leo kuwa hawana akili? Akili zao ni kama zilivyoelezwa na yuleeee kocha wao aliyeondoka na kuwapa majina fulani fulani. Lkn, waandishi wetu pia ni wa ovyo kweli: professionalism (na elimu) zao wengi huwa zinatupa maswali mengi mno! Wapo wale wenye kazi ya kuandika habari za uongo na za kutunga ili kuuza magazeti. Ukiwa kwy journalism na ukapata mafunzo stahiki, kisha ukiwa kazini ukachunga ethics zake, huwezi kuleta vioja kama wafanyavyo baadhi ya "waandishi" wetu. Kwa nini hawakujitahidi wapate angalau picha tu ya hiyo "nyumba" ya Chama aliyojengewa? Juzi kati ikaja pia habari kwamba eti Chama anataka "kuhakikishiwa" usalama wake akitua Yanga! Ujinga mtupu! Waandishi wa aina hii wanapaswa kubadilika..na pa kuanzia, wanapaswa waende rasmi kusomea fani inayoitwa Journalism. Hii ni fani yenye heshima zake, si ya kuvamia kwa sababu ulikosa kitu kingine cha kufanya maishani mwako.


      Delete
  5. Kuweka uso chini haikuhusu, kwani wewe unaweza kusaini huku macho yakiwa yanaangalia angani?

    ReplyDelete
  6. Wewe ndio mbumbula baada ya akili nadhani unakinyesi kwenye bongo yako.Yaani ulitaka chama wakati anasaini mkataba awe anatizama hewani? Angejua kweli anachokisaini? Ukitaka picha za ziada kwenye zoezi hili la chama kusaini nenda kwenye YouTube kunapicha tele.

    ReplyDelete
  7. Tulishazoea maneno yenu kila Sikh chama kasaini , ndani ya msimu huu 2020/2021 kasaini zaidi ya Mara 3 ? Mtuambie atakuwa msimbazi miaka mingapi?

    ReplyDelete
  8. Inaonesha wewe ndie dalali anaemtafutia Chama wateja. Ikiwa Moo alieahidi kumleta mchezaji wa bei yoyote kukipa nguvu kikosi chake vipi leo hii wafanikiwe yanga kumchukuwa Chama wakati ambapo walishindwa kumnunuwa Sure Boy wa Azam wawe leo hii iwe na uwezo wa kumtowa Chama kutoka mikono mwa Moo? Ikiwa Chama ataondoka basi atakwenda kwa wale wenye uwezo kama uwezo wa waliomchomoa Sven lakini sio yanga

    ReplyDelete
  9. Ukuma tu huu Kwan hakuna mchezaji bora kuliko CHAMA? Arafu simba kuweni na akili kwamba hata CHAMA ipo siku ataondoka tu na maisha yataendelea kwingine

    ReplyDelete
    Replies
    1. KUNA MTU ALISEMA CHAMA HAONDOKI? KILA MTU ASHINDE ZAKE

      Delete
  10. Moo alisema Chama amesha saini, Sasa Povu la nn?
    ��������

    ReplyDelete
  11. Admin wa blog muwe mnaondoa na kublock watu wanaopost matusi. Hui sio uwanja wa fisi ambapo kila mlevi anaropoka ovyo tuu. Kuna watu wenye heshima zao humu

    ReplyDelete
  12. Ko chama anaendelea kuwatumikia mikia fc? a.k.a Watumwa wa mwamedi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama vile nakuona huamini! Chama alikuwa anasikilizia tu kama timu itaingia makundi ya CAF Champions League, isingeingia alikuwa anaondoka zake kwenda mbele, ila sio Yanga

      Delete
    2. Msijisahaulishe jamani. 'Watumwa' wa Mwamedi sawa, ila msiwasahau wale watumwa wa ...waliokuwa wakibeba watu mabegani pale airport..ile ndio taswira asilia ya utumwa.

      Delete
    3. Na nyie watumwa wa GSM mtaacha lini kumbeba bwana mdogo kwenye machela!

      Delete
  13. Watumwa wanajulikana walianza kwa kumpigia magoti Manji pucha za ushahidi zipo.
    Wakambeba mfanyakazi tu wa GSM tena msomali koko kwenye machela kana walivyolazimishwa watwana enzi za utumwa.
    Hivi Utopolo nani anawabebea ubongo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tena dogo akawafanya wawe wanakesha kuwapokea wanariadha uwanja wa ndege!!! Bado wanajiona wana akili...Kweli Uto ni Uto tu

      Delete
  14. Ile nyumba ya barafu mliomjengea Chama huko Zambia imeyeyuka?
    Mwakalebela na msanii Nugaz wanawajulia misukule ya Utopolo kila upande wanawageuza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni aibu kwa kiongozi mkubwa kama Mwakalebela kutuaminisha wanaYanga kuwa Chama anakuja Yanga. Ni jambo la hovyo kwa Dismas Ten kutuwekea video ya Chama akilitangaza jarida la Yanga. Ni kujitoa fahamu kwa Nugaz kutuhakikishia Chama keshasaini Yanga and time will tell ni timu ipi inammiliki Chama

      Delete
  15. Wavunje benki wakati wameshamjengea nyumba!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic