February 17, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa matokeo ambayo wameyapata leo ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo na imetokana na wachezaji wao kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza na cha pili.

Ikiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa ilikubali sare ya kufungana mabao 3-3 mbele ya Kagera Sugar na kugawana pointi mojamoja.

Ni Kagera Sugar walianza kufungua akaunti ya mabao dakika ya 10 kupitia kwa Peter Mwalanzi na lilidumu kwa muda wa dakika nne ambapo Yanga waliweka mzani sawa dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Tuisila Kisinda.

Hasan Mwaterema alitumia dakika 9 kuandika bao la pili kwa Kagera Sugar na lilidumu dakika 6 kwa Deus Kaseke kuweka usawa dakika ya 29.

Ikiwa kwenye dakika zile za nyongeza kukamilisha dakika 45, nyota wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu alipachika bao la tatu dakika ya 45+ 1 na kuwafanya Yanga waende mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja.

Kipidi cha pili Yanga walikuja kwa kasi na kupachika bao la usawa dakika ya 60 kupitia kwa Mukoko Tonombe kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulikuwa unasoma 3-3 na timu zote zimegawana pointi mojamoja.

Kaze amesema:"Ni makosa yetu kushindwa kukamilisha mchezo ndani ya kipindi cha kwanza na cha pili kwa kuwa tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia hivyo hakuna wa kumlaumu katika hili,". 

Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wametoa burudani na mabao wamefunga.

16 COMMENTS:

  1. Timu ya Yanga isahau ubingwa mwaka huu.

    ReplyDelete
  2. Wanataka ubingwa harafu mfungaji ndo sapongo

    ReplyDelete
  3. Ndio soka, mpira ni mchezo wa makosa ukikosea ndio Furaha/ advatage kwa mwenzako, mechi bado nyingi, anything can happen,
    Hata Simba sio kama hawakosei ni suala la muda tu, muda utaongea

    ReplyDelete
  4. Yaan tofauti ya point chache hivyo Kisha wasahau ubingwa, tuache ushabiki wa kizamani team lazima ushinde kila mchezo ndio uchukue ubingwa, ligi bado ni ndefu, hata ingekua tofauti ya point 10, bado huwezi kitabiri bingwa, Tukumbuke ligi ya mwakahuu hakuna team inayoachia point kirahisi, team nyingi zimejipanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyinyi si mlikuwa mnajiita mabingwa kwani mlikuwa hamjui ligi ni ndefu

      Delete
    2. MDAU ACHA KUJIPA MOYO, MUULIZE NUGAZ KAMA MTATWAA UBINGWA AU LA! MAANA NAONA SARE SARE ZIMEANZA UPYA NINI TATIZO? HAMLI AU MNAUGUA? YULE MCHEZAJI WENU BORA WA MWEZI DECEMBER KAENDA WAPI?

      Delete
  5. Sababu hazishi kila siku pukutisha point, zikowapi mashine za magoli tulizoahidiwa. Wachezaji kama wanaumwa na wasio na furaha na. Shishimbi mlimuacha bure kuonesha kama mliotaka kumkomoa. Hali ya timu inatuumuza sana

    ReplyDelete
  6. Jiulizeni maswali kwanini shishimbi amesajiliwa as vita alafu kisinda na mukoko wametolewa kwa mkopo? Alafu jamaa anacheza first eleven sasa,kama mna akili Jiulizeni kwanza hilo swali mkipata jibu basi mtakua mmepata pia jibu la ubingwa msimu huu,mlikua mnajiita mabingwa ghafla mnaanza kutetema.endeleen kujiita mabingwa kwasababu bado mnaongoza ligi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaongeleaga shishimbi anayepata nafasi ya kucheza kwa bahati 2

      Delete
  7. Tulikuwa tunalia kwa matokeo mabaya pale alilpoondoka Manji lakini sasa tunaye kuliko Manji na wachezaji na baraza la ufundi pia ni bora kuliko siku za Manji lakini juu ya hivo matokeo ni yakuvunja. Uko wapi uwezo wa Mwanyato sasa ulinzi ndio inayoyoruhusu magoli na na mastraika ndio wanaotunyima msgoli

    ReplyDelete
    Replies
    1. DK 45 TIMU INA RUHUSU GOLI 3, INACHEZA MECHI 2 INAPATA POINT 2, INAFUNGA MAGOLI 4 NA INAFUNGWA MAGOLI 4. HII NDIYO ILE TIMU ITUNAYOAMBIWA KUWA INA DEFENCE IMARA, WASHAMBULIAJI BORA WAMECHEZA ULAYA WENGINE. NDIYO TIMU AMBAYO TUNAAMBIWA INA KAA KAMBI YA GHARAMA SANA HAPA BONGO KULIKO HATA YOYOTE. NDIYO TIMU TUNAYOAMBIWA KUWA INA WACHEZAJI VIJANA WENGI WENYE VIPAJI LUKUKI...WENZENU SIMBA WANARINGIA WAZEE WAO!

      Delete
  8. Yunajivunia ni kuwa ni yanga tu mpaka sasa hapana timu katika ligi iliyothubutu kuifunga na hii ni fahari kubwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. SEMA HIVI HATUJAPOTEZA MCHEZO MDAU, TIMU IMERUHUSU GOLI 3 NDANI YA DK 45 UNASEMAJE HAIFUNGWI?

      Delete
  9. Mungu hadhihakiwi bwana, juzi walisema MBEYA CITY kapewa penati isiyo ya halali, hatimae penati kama ile eneo lilelile na wao wamepata penati je inamaana nayo haikua penati? Tatizo la madimbwini mnaongea sana alafu uwanjana hamna lolote, poleni sana mungu atawalipia deni subirin muda ufike tu.

    ReplyDelete
  10. Yani penati zinafanana kama vile mungu alijua ili awakate ngebe wakome kuropoka, yanga mnaongea sana punguzeni jamani mtaaibika jamani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic