DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, utakaochezwa Uwanja wa Karume, Mara.
Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 imeachwa kwa jumla ya pointi 7 na watani zao wa jadi Yanga ambao wapo nafasi ya kwanza na pointi 46.
Yanga imecheza jumla ya mechi 20 huku Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 kwa msimu wa 2020/21 ambao umekuwa na ushindani mkubwa.
Gomes amesema:"Ninawatambua Biashara United ni moja ya timu bora na imara ikiwa ndani ya uwanja kwa namna ambavyo inacheza na kutafuta ushindi.
"Wanacheza vizuri hilo lipo wazi ila ninaona nami kikosi chetu kipo imara hasa baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa AS Vita nchini DR Congo jambo ambalo linatuongezea nguvu ya kujiamini,".
Francis Baraza, Kocha wa Biashara United amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji kupata pointi tatu ndani ya uwanja.
Kocha huyo ameweka wazi kuwa wachezaji wake wote wana nafasi sawa ndani ya uwanja hivyo hakuna mwenye namba ya kudumu kikosi cha kwanza hivyo kesho kunaweza kuwa na mabadiliko kikosi cha kwanza.
Miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kuonyesha makeke yao ni pamoja na kiungo Ibrahim Ajibu, Said Ndemla na Hassan Dilunga ambao hawajawa na nafasi chini ya Gomes.
0 COMMENTS:
Post a Comment