MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wapo
tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kuwa
wanazitaka poiti tatu.
Kagera Sugar, Februari 11 ilikamilisha kwa kupata sare ya
kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Kaitaba inakutana na Yanga
iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa
Sokoine.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 17 Uwanja wa Mkapa
unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza
Kagera Sugar ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na Saleh Jembe Maxime amesema kuwa wapo
tayari kwa ajili ya mechi zao zote za mzunguko wa kwanza na wanaamini kwamba
watapata pointi tatu muhimu.
“Kwenye mechi zetu zote ndani ya uwanja tumejipanga kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu hivyo mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga nao ni sehemu ya mchezo, tutaingia kwa kuwaheshimu ila tunazihitaji pointi tatu.
"Mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani ushindani ni mkubwa na wapinzani wetu nao sisi tunawaheshimu hivyo,".
Itakuwa ni aibu kwa Kagera kutowafunga Yanga hasa ukifikiri hivi juzi tu waligaragazwa na African Sports na baadae droo na Mbeya City. Wataingia uwanjani nao wana hofu ya kufungwa tena na hiyo itakuwa fursa kubwa ka Kagera
ReplyDeleteWee acha yako. Engineer Hersi amemuona. Njaa yao ndio kifo chao. Tutampiga Kagera 2-0. Japo magoli ya ajabu lakini lazima tushinde na sisi mwakani tupande ndege
DeleteWewe huwa unaota hata mchana, siyo?
DeleteSALEH TUNAKUANGALIA TU IPO SIKU YAKO
ReplyDeleteYanga lazima tushinde hata kama ni kwa ushindi wa magoli ya ajabu ajabu
ReplyDelete