February 16, 2021

 

UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Namungo umesisitiza kuwa kile kilichofanywa na wenyeji wao nchini Angola, Clube Desportivo 1º de Agosto, si fitina za soka bali ni uhalifu wa kupanga ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Namungo ilirejea nchini jana usiku baada ya mchezo wao wa mtoano hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya de Agosto uliopaswa kupigwa juzi Jumapili kufutwa.

Mchezo huo ulifutwa baada ya kuibuka mvutano mkubwa, baada ya nyota watatu wa kikosi hicho pamoja na kiongozi mmoja kudaiwa wana maambukizi ya Corona.

Kufuatia mvutano wa mamlaka mbalimbali za nchi zote mbili kwa kushirikiana na Shirikisho la soka Afrika (CAF), mchezo huo ulifutwa ili kupisha uchunguzi wa sakata hilo chini ya kamati maalum ya CAF.

Akizungumzia sakata hilo, Ofisa habari wa Namungo Namlia amesema: “Timu imelazimika kurejea nchini bila wachezaji wake watatu na kiongozi mmoja ambao kimsingi kutokana na sheria za mamlaka ya afya wao wataendelea kubaki mpaka pale watakapokuwa wamepona.

“Tunaendelea kusubiria maamuzi ya CAF lakini kiukweli kitu walichokifanya wenyeji wetu sio fitina za mpira kama ambavyo watu wengi wanalichukulia, bali ni uhalifu wa kupanga ambao umeshirikisha mamlaka mbalimbali za nchi hiyo,"

 

 

4 COMMENTS:

  1. Ni kweli ni uvunjaji wa haki za binaadamu. Nasisitiza hili suala sio la kuacha hivi hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhan Namungo wamefanya kosa kukubali kuwacha hao wachezaji 3 na kiongozi wao! Coz waangola watafanya kila njia kuthibitisha kwamba wana maambukizi ya Corona, ili kukwepa rungu la CAF.
      Wangerudi nao kuzuia hujuma.
      Safari nyingine Namungo wazingatie kwamba soka kwa hatua waliyofikia ni biashara/ pesa na fursa ya kuongeza uwakilishi wa nchi.
      Wasafiri na viongozi wa ngazi za juu na wataalamu wa fitna sio huyi Zidadu pekee

      Delete
    2. Kosa si la namungo. Kama wachezaji watatu wanakorona Basi wale 27 wangecheza. Hivyo namungo anaweza kupata point za bure

      Delete
  2. Anapenda kufahamu Hivi sheria za CAF zinasemaje team ikikutwa na baadhi ya wachezaji wanaCorona?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic