MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, FISTON Abdoul Razack, ametamba kuwa anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika michezo iliyo mbele yao na kumaliza tatizo la matokeo ya sare mfululizo.
Nyota huyo alisajiliwa na kikosi cha Yanga katika kipindi cha dirisha dogo, ambapo mpaka sasa ameichezea Yanga michezo miwili akiwa bado hajafunga bao lolote.
Akizungumzia malengo yao Fiston amesema:"Kila mmoja amesikitishwa na matokeo tuliyopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, na tumedhamiria kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika michezo yetu ijayo kwa kuwa malengo yetu ni kutwaa ubingwa,"
Yanga kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza dhidi ya Kagera Sugar, ambapo matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda kwa bao 1-0.
Fiston alitakiwa kuanzia bench ili azoeane na wenzake kwanza. Kumpa aanze kucheze dakika 70+ haitasaidia timu.
ReplyDeleteMajigambo ya kwenye media lakini uwanjani hamna kitu
ReplyDeleteFISTON NI MCHEZAJI WA KAWAIDA SANA ILA MAGAZETI YA KIBONGO, WACHAMBUZI UCHWARA WA SOKA, WAMEMPA BIG HEAD. CAREER PROFILE YALE KATIKA KLABU ZOTE ALIZOCHEZA NI MAGOLI 15 TU NA HAPO ANA MIAKA 27. UNAWEZAJE KUSEMA KUWA MMESAJILI MCHEZAJI BORA, MTAMBO WA MABAO,NA MAJIGAMBO RUNDO YASIYOISHA? HEBU MTZAMENI MK14 AMEKUJA SIMBA BILA KELELE, ANGALIA KAZI ANAYOIFANYA.
ReplyDeleteWanaonyanyuwa kumpa umaarufu utafikiri keshatia goli angali moja au kama wanavofanya akina Muguli, Balwa, Chama au Morrisoooon
ReplyDeleteKweli hajatuonyesha tulichotarajia, mechi na African Sports halafu Mbeya City zote amecheza kawaida sana. Nilitaraji japo kuona uwezo binafsi sikuuona. Ntabazonkiza alianza vizuri zaidi,ukilinganisha na Fisyon. Kuna wakati nawaona Kaseke na Farid kama bora zaidi ya baadhi ya wageni tuliosajili.
ReplyDeleteWw ni shabiki wa kweli kwenye mpira lazima useme ukweli ili usipate stress kweli hajaonyesha cheche zozote ila yanga wampe muda anaweza kuonesha kitu ila tuache tabia ya kutukuza wachezaji kabla hawajacheza uwanjani tunawapa wakati mgumu wachezaji na presha ya juu na wanashindwa kurelax kwasababu ya presha ya ,mashabiki
ReplyDelete