SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi kuachana
na kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Etienne
Ndayiragije kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa habari wa TFF Clifford Marion Ndimbo amesema wanamshukuru kocha huyo, na tayari mchakato wa kumsaka mbadala wake umeanza ambapo atatangazwa muda wowote kuanzia sasa.
“Baada ya kikao cha pamoja na kocha Etienne Ndayiragije, pande
zote mbili zimefikia makubaliano rasmi ya kuvunja mkataba.
“Tunamshukuru kocha Ndayiragije kwa kazi yake kipindi chote
alichoifundisha Stars, mchakato wa kumtangaza mbadala
wake unaendelea na atatangazwa muda wowote kuanzia sasa,”
Hii hapa taarifa ya TFF;
daaaa kiujumla cjaona tatizo la kocha,,,mi nafkl bado hatuna wachezaji bora na welevu,,,wenye natamanio katka fani yao,,,ukiangalia hata ligi yetu bado timu zetu zinabebwa na wachezaji ,,,tutalaumu sana makocha ila bado tz hatuna wachezaji muhimu kwenye kila idara
ReplyDeleteTFF wapo sawa kabisa kuachana na kocha ndayiragije tena wamechelewa kufanya hivyo.Tatizo la Tanzania linaanzia kwenye vyombo vyetu vya habari vya michezo, vyingi vina Wachambuzi wanaopotosha umma au kuwa na nidhamu ya uoga linapokuja juu ya Suala la kocha wa timu ya Taifa.Hivyo ni lini hasa taifa Stars imefundishwa na kocha mwenye vision au mitizamo halisi kwenye falsa ya tamaduni ya soka fulani? Ni lini hasa Taifa stars ilisha fundishwa na kocha alieshinda angalau ubingwa wa ligi husika au kombe husika kwenye ligi fulani kubwa ya ushindani angalau barani Africa? achana na ulaya. Kwa takribani miongo kadhaa sasa Makocha wanaoteuliwa kuja kuifundisha Taifa stars ni wale Makocha wanaotaka kupata uzoefu wa kufundisha timu za Taifa basi. Tatizo letu Tanzania na chama chetu Cha mpira Ni uvivu wa akili wa kushindwa kufikiri nje ya maeneo yetu ya akili za kawaida na inashangaza kumsikia mtu anaejiita mchambuzi akisema bila ya kufikiri kwamba Kuna umma wa watanzania wapenda michezo wanaomuamini wanamsikiliza,ati hata akija Gwadiola timu yetu ya Taifa haiwezi kufanya vizuri?Yaani unamfananisha Gwadiola na kocha Ndayiragije au Mkwasa au Amunike au Mgunda au Ame Ninje? Maana hao ndio makocha wetu wa Taifa stars. Ukienda kule ushokani ama east Europe Kuna watu wa kazi kwenye soka na si wa gharama wa hivyo chakushangaza Taifa stars ipo kwenye kuokotezaga makocha zaidi kila leo wasio na malengo.Falsafa ya mpira wa leo ni mpira wa Kasi na nguvu ila kwa makocha hawa wa Taifa stars watanzania tutarajie kuendelea kupata maumivu zaidi.
DeleteNa asikudanganye mtu kwamba kocha sahihi hana impact kwenye kubadilisha ubora wa timu na mchezaji mmoja mmoja. Ukweli ni kwamba unaweza kuwa na wachezaji wazuri tena Sana lakini bila ya kocha sahihi timu ikashindwa kufikia malengo.Na unaweza ukawa na wachezaji wabovu tena Sana lakini ukawa na kocha sahihi timu ikafikia malengo na kushangaza watu. Unaweza kusema kwenye mpira kocha ndio kichwa Cha mwili wa mpira Yaani bila ya kocha hakuna mpira. Kazi ya kocha sio changamoto ya uwanjani tu, bali vipi anaishauri mamlaka ya soka husika bila ya uoga pale kwenye Jambo la msingi. Na Kama kuna taasisi fulani ya soka iliozoea magumashi inaweza kuajiri kocha anaewaabudu mabosi wake pia bila ya kujali taaluma yake ila mwisho wa siku mpira ni mchezo wa hadharani.
Hapo bado hakuna point yoyote, usifikir makocha wakubwa wanapata umaarufu kwa CV pekee, pekee bali lazima uwe nakikosi kizuri, sidhani kama marekani, china wangeshindwa kufanya vzr kwamaana wanauchumi bora wakumpata kocha bora yoyote, kikubwa mfumo wakuandaa wachezaji wetu ndio shida, mm nawatabiria uganda kama wataendelea nautaratibu wao huu wakuzallisha vipaji watakuja kuwa twifa lakusumbua afrika
Deletedaaaa kiujumla cjaona tatizo la kocha,,,mi nafkl bado hatuna wachezaji bora na welevu,,,wenye natamanio katka fani yao,,,ukiangalia hata ligi yetu bado timu zetu zinabebwa na wachezaji ,,,tutalaumu sana makocha ila bado tz hatuna wachezaji muhimu kwenye kila idara
ReplyDeletedaaaa kiujumla cjaona tatizo la kocha,,,mi nafkl bado hatuna wachezaji bora na welevu,,,wenye natamanio katka fani yao,,,ukiangalia hata ligi yetu bado timu zetu zinabebwa na wachezaji ,,,tutalaumu sana makocha ila bado tz hatuna wachezaji muhimu kwenye kila idara
ReplyDeletedaaaa kiujumla cjaona tatizo la kocha,,,mi nafkl bado hatuna wachezaji bora na welevu,,,wenye natamanio katka fani yao,,,ukiangalia hata ligi yetu bado timu zetu zinabebwa na wachezaji ,,,tutalaumu sana makocha ila bado tz hatuna wachezaji muhimu kwenye kila idara
ReplyDeletetimu zetu bado zina bebwa na wachezaji wa kigeni
ReplyDeleteAcha kutujazia povu humu....comment moja inatosha sana sio kurudia rudia kutuma comment moja nne au zaidi
DeleteKikubwa viongozi wetu wampira wanafanya kazi/maamuzi kwakuwasikiliza mashabiki, sijaona kosa la ndairagije, zaidi namsifu kwakuanza kuingiza damu changa kikosini, pia ukitazama hao ndio wachezaji wetu wanaofanya vema ndani ya ligi yetu, sasa unamfukuza kocha kwabaya lipi?
ReplyDeleteAende Azam fc maana bado pengo lake linaonekana
ReplyDeletekiukweli kabisa sisi bado kabisa kimpira nayakumbuka sana maneno ya muheshimiwa rais mstaafu wa awamu ya pili mzee mwinyi aliposema tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
ReplyDelete