KOCHA wa Simba, Didier Gomes, amefanikiwa kuvunja rekodi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems maarufu kama uchebe baada kucheza mechi mbili za ugenini katika hatua ya makundi bila ya kupoteza.
Gomes amevunja rekodi hiyo baada ya kujiunga na Simba akitokea Al Merrikh ya Sudan ambapo hadi sasa hajapoteza mchezo wowote katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, imecheza mechi tatu, ikifanikiwa kushinda mbili na kutoka sare moja.
Chini ya kocha huyo raia wa Ufaransa, Simba ikiwa ugenini, imeshinda dhidi ya AS Vita, kisha ikatoka suluhu na Al Merrikh ambayo imekuwa ni rekodi tofauti na wakati wa Aussems msimu wa 2018/19.
Katika msimu wa 2018/19, licha ya Simba kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, lakini haikushinda mchezo wowote wa ugenini hatua ya makundi ambapo ilifungwa mabao 5-0 na AS Vita, kabla ya kufungwa tena na Al Ahly mabao 5-0, huku ikichapwa 2-0 na 2-0 na JS Soura.
Jumanne, Simba ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh ambapo utakuwa ni mchezo wa pili kwa Gomes kuiongoza Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa.
0 COMMENTS:
Post a Comment