March 11, 2021


 DIDIER Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mbali na wachezaji wake kukosa penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons bado walikosa nafasi nyingi za wazi jambo ambalo watalifanyia kazi.


Wakati ubao ukisoma Simba 1-1 Tanzania Prisons,  Chris Mugalu alipiga penalti iliyoishia kwenye mikono ya kipa namba moja wa Prisons,  Jeremiah Kisubi.


Jitihada za Simba kutafuta bao zlikuja kuonekana dakika ya 90+5 kupitia kwa Luis Miquissone na kufanya Simba ipate pointi moja kwa kuwa ilifungwa dakika ya 56 na Salum Kimenya kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18.


Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa wamekuwa wakifanyia mazoezi mipira iliyokufa mara kwa mara ila imekuwa ngumu kwao kupata ushindi jambo ambalo atalifanyia kazi wakati ujao.


"Ukiachana na kukosa penalti bado wachezaj walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia hivyo ni kazi kwetu kuyafanyia kazi makosa kwa ajili ya wakati ujao.


"Kukosa ama kupata kwetu ni darasa kwa ajili ya muda mwingine.  Nina amini kwamba kuna kitu ambacho wachezaji wamekipata na wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana, ".


Simba inafikisha pointi 46 ikiwa nafasi ya pili huku vinara ni Yanga wana pointi zao 50 kibindoni.

6 COMMENTS:

  1. Kukosa nafasi sawa ila viongozi wa Simba wanatakiwa kuwa makini zaidi kipindi hiki kwani wasipokuwa makini Simba itatumika kuwafariji Yanga na shida za migogoro yao.Tunajua Simba wana watu makini katika kukabiliana na fitina ila mechi za ligi ziwe na mikakati yake maalum isiwe maneno tu.Simba ikifanya vizuri kwenye ligi kuu ndiko kutajenga kujiamini zaidi klabu bingwa Africa. Kocha haingiliwi ila anahitaji kuwa na washauri sahihi na ni wakati sahihi sasa kocha wa Simba akashauriwa kumuingiza Morrison kwenye first even. Morrison anaecheza na majukwaa ila Majukwaa hayamchezeshi Morrison na huwa anaecheza mpira kweli kweli uwanjani.Kuna watu wanatamani kumuona Morrison anapotea kabisa si uwanjani tu bali hata maishani Simba wanatakiwa kufahamu hilo.Na si kutamani tu bali Kuna watu wanafanya kazi ya kumpoteza Morrison katika masuala ya soka kwa hivyo kitu kidogo kwake kibaya akikifanya au kumtokezea au hata kuzushiwa tu huwa ni kitu kikubwa kupita maelezo kwenye mtazamo ghasi hata Kama haistaili kuwa hivyo.Kuwaonya tu Simba hata hiyo mechi ya Elmereikh ya marudiano hapa nyumbani yaweza kuwa ngumu kuliko ile mechi ya awali kule Sudan. Simba wanatakiwa kuwa makini kipindi hiki kwani kuja kuzipita point za Yanga haitakuwa Jambo rahisi na si kwa sababu za kimpira bali ni figisu na huko nyuma Yanga walifanikiwa kuwa bingwa kwa staili hii na matokeo yake Tanzania tunakuwa na wawakilishi wa kimataifa waliotepeta.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko sawa mdau huu ni muda wa kuwa makini sana, maana Ukiangalia michezo miwili iliyo pita ya Simba, unapata ushahidi wa ulichozungumza.

      Delete
    2. Kabla ya Mchezo wa juzi wa Simba tulikuwa tunnafuatilia maandalizi ya timu zote mbili na baadaye kulinganisha kilichofanyika uwanjani na matokeo na kubaini Simba inatakiwa kuongeza umakini zaidi hasa kipindi hiki kwani zile rafu na ukamiaji ule wa kuhatarisha maisha ya wachezaji wengine ni za kuchungwa.

      Delete
  2. Acha unafki wewe bwege, huwezi kutoa maoni yako mpaka uitaje Yanga? sasa hapo Yanga anaingiaje? toa maoni yako kwa club yako nn kifanyike ili muweze kuendelea kufanya vizuri hata kwenye mechi za ligi. Yaani manara ameshawaharibu hawa watu hawa. Hawawezi kutoa tathmini za tim yao mpka muitaje Yanga. Mbona mnaposhinda kima taifa hamuitaji Yanga? Acha umbumbu mbu wako wewe. hakuna asiejua nyinyi ndio mnaongoza kwa kuhonga marefa, na mnahonga mpka Tim pinzani ili zikazie Yanga kama mlivyofanya kwa kagera na coast. Jana refa kazidisha muda na akawapa na goli la of side. bado hamridhiki tu,bado mnaweweseka kua Yanga ndio mchawi wenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mhh ulichoandika unakijua mwenyewe maana hayo maharage uliyokula nahisi ni ya juzi.Ubingwa nyie Utopolo a.k.a.Vyura hamchukui na mtaendelea kutepeta kama mlenda

      Delete
  3. Umesema vizur; Morrisson anatakiwa awe kwenye first eleven anauwezo wa ku pressurize, ana control and everything.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic