DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa taarifa ambazo zinaeleza kwamba ana ugomvi na mchezaji wake Bernard Morrison zimemsikitisha kwa kuwa wanaishi wakiwa ni familia ndani ya timu.
Hivi karibuni imekuwa ikielezwa kuwa kocha huyo raia wa Ufaransa hawaivi chungu kimoja na Morrison jambo ambalo lilimfanya amuweke kando kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao ulikuwa ni wa ligi.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 3-0 JKT Tanzania baada ya dakika 90 na nyota huyo hakuanza kwenye mchezo huo.
Pia kwenye msafara wa Simba ambao uliibukia nchini Sudan kumenyana na Al Merrikh mchezo uliochezwa Machi 6 na ubao kusoma Al Merrikh 0-0 Simba baada ya dakika 90, Morrison aliachwa Bongo.
Gomes amesema:"Kuhusu kuwa na ugomvi ni Morrison pamoja na kutoelewana nayo hiyo sio kweli kwa kuwa nimekuwa nikizungumza naye vizuri.
"Pia sisi tunaishi tukiwa ni familia hakuna ambaye anamkasirikia mwenzanke, kuhusu kubaki hilo siwezi kutaja sababu kwa kuwa mwalimu anajua aina ya wachezaji ambao anawahitaji ila hakuna ugomvi kati yangu na Morrison," .
Morrison aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu ya Yanga ambapo amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Simba tangu zama za Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga.







msiondoe habari mtandaoni kwa kuwa wadau wameposit yale msiyopenda..
ReplyDeleteNi kweli baada ya Yanga kuanza kusua sua mliamua kuacha kuwa mnaweka msimamo wa ligi
wakati ikiwa inashinda kwa kibao kimoja mlikuwa mnaweka msimamo hadi mara mbili kwa wiki..
Tulitaka kushukuru tu leo kwa kutuwekea msimamo wa ligi..mara mmeishusha..Sasa hakuna asiyejua ni Azam anampumulia Yanga. Bado point 4 na FA cup kwa mwendo huu, Yanga hachomoi
Hali Ni Tete Bado kidogo utasikia mwenyekiti out
ReplyDeleteDa Rosa Hana sakata na Morrison. Sema uzushi ndugu mwandishi.
ReplyDeleteKwa Morrison Simba Kuna tatizo viongozi wasitudanganye
ReplyDeleteThat's poor performance of ur' football clubs
ReplyDeleteHaya mke wa Morisson tuambie tatizo ni nini?
ReplyDeleteUongozi wa Simba na kocha wamesema hakuna tatizo inaelekea wewe unajua zaidi tujuze.