March 13, 2021


 BEKI kisiki wa kati wa Klabu ya Simba, Joash Onyango amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kushinda kwenye mechi zao za nyumbani kimataifa ili waweze kufikia lengo la kutinga hatua ya robo fainali.

Baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana Machi 6, mbele ya Al Merrikh, Machi 16, Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya wapinzani hao kutoka Sudan, Uwanja wa Mkapa.

Ikiwa ipo kundi A na pointi 7 inaongoza kundi inakutana na wapinzani wao ambao wapo nafasi ya nne na pointi moja ambayo waliipata mbele ya Simba.

Onyango ameshuhudia makipa wake wawili, Aishi Manula na Beno Kakolanya hatua ya makundi wakitoka bila kufungwa kwenye mechi zote tatu, ambapo Manula mechi mbili na moja Kakolanya amesema kuwa bado kazi inaendelea na watapambana kupata matokeo.

“Kwetu sisi mpango namba moja ni kupata ushindi uwanjani na mwalimu ametuambia kwamba kwa mechi za nyumbani kwetu ni muhimu kushinda ili kupata pointi tatu ugenini tukipata sare sio mbaya ila kikubwa ni kupambana ili kufika hatua ya robo fainali.


"Ushindani ni mkubwa nasi hilo tunalitambua hivyo tunaingia kucheza tukiwa tunajua hali halisi ya kile ambacho kinatakiwa. Kikubwa ni ushindi na kuweza kuwapa furaha mashabiki ambao wamekuwa wakitupa sapoti kila wakati," .


Onyango ni ingizo jipya ndani ya Simba kutoka Klabu ya Gor Mahia ameweza kuingia moja kwa moja kikosi cha kwanza akishirikiana na Pascal Wawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic