UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Merrikh, Machi 16 hakutakuwa na ruhusa ya mashabiki kuingia kuipa sapoti timu hiyo.
Licha ya kwamba kulikuwa na katazo la mashabiki kwa timu nyingi ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ila kwa Simba walikuwa wanapata kibali cha kuingiza nusu ya mashabiki.
Hii ilikuwa ni kwa sababu ya kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.
Leo Machi 13, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wakati wakiwa kwenye maandalizi ya mechi hiyo itakayokuwa na ushindani mkubwa wamepokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwamba hawataruhusiwa kuwa na mashabiki.
"Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini sikumbuki kama hapa nchini tumewahi kucheza bila mashabiki. Tunawaomba radhi mashabiki kwa mechi hii sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika.
"Tukiwa kwenye maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Al Merrikh hapo tulipokea taarifa kutoka TFF kwamba hatutaruhusiwa kuwa na mashabiki, hivyo hii ni taarifa mashabiki wetu watuwie radhi.
"Watakaoruhusiwa kuingia ni watu wachache hasa wale ambao wanahusika na maandalizi ya mechi lakini maandalizi yapo vizuri na tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa," .
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Machi 6, Simba ililazimisha sare ya bila kufungana ikiwa ugenini, ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali.
Kibindoni kwenye kundi A ina pointi 7 inakutana na Al Merrikh ikiwa na pointi moja.
Je wale paka wetu wataruhusiwa kuingia?
ReplyDeletekwani shida nini? si na gongowazi wawatumie. kwani matopeni hawafugi paka.unashinda unalalamika kila siku pata...tuhuma eti ndio waliomfikisha simba makundi...paka ndiyo wanafanya simba ashinde...Kwani Yanga wao hawataki bil 1.6 za CAF au wanataka poteza mwaka wa nne bila ubingwa...kama paka wanasaidia na Yanga pia wawatumie
ReplyDeleteHizo 1.6 Bil unafikiri ata senti tano utaiona? Mmesahau timu mmeuza? Jamaa kashabadili logo. Nenda pale Msimbazi kama utaona Ofisi ata ya Manara!
ReplyDeleteAah aahh!!! Akili ni neno pana sana ila kiufupi huyu gongo waz niseme tu hana akili na hana akili kwa kuwa ameshindwa kuztumia ipasavyo ivi unahisi hixo pesa ama hyo ofisi ww au mimi inatusaidia nin zaidi ya wanaoendesha club na wanachama na lama hana ofisi haji taarfa zake anaandalia wapi nyumban kwake au vichocholon ebu tumia akili kama washabiki kazi yetu kuona timu ikifanikiwa na tukipt habar kwa njia yoyot ile..na sio pesa kwa sabab simba hawatafut pesa kwa ajili ya shabiki ..mbona nyie ombaomba mmechangia litimu lenu mwisho mmeshindwa now dz mnasaidiwa na mpga dili wenu gsm asiyejulikana amekuwa pale kama nani mwekezaji au mfadhili au mfanyabiashara ?? Msije mkaturudisha nyuma enzi za kutawaliwa mkiona kama mnasaidiwa kumbe mnanyonywa..wakumbukeni vitanguliz vya ukoloni vilikuja kwa staili gani na mwisho wa siku ilikuwaje..so we feel proudly to see simba on top..on high level in and out of tz thats very nice thing for simba fans..
DeleteKwani vita kule kwao aliguswa na mashabiki
ReplyDelete