March 10, 2021


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kuna umuhimu wa watani zao wa jadi Yanga kukubali kwamba ni lazima wajiimarishe kwenye uongozi kabla ya kuanza kufikiria mafanikio ya haraka.

Kwa sasa Yanga imefuta makocha wawili ndani ya msimu mmoja ambapo ilianza na Zlatko Krmpotic ambaye aliongoza timu hiyo kwenye mechi tano, alishinda nne na sare moja akafutwa kazi.

Machi 7, Cedric Kaze ambaye alikuwa mrithi wa mikoba ya Zlatko naye alichimbishwa akiwa ameongoza kwenye mechi 18 za ligi, alishinda 10, sare saba na kichapo mechi moja.

Tayari Yanga imemtangaza Juma Mwambusi kuwa kocha wa Yanga wakati wakiendelea na mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye ataendelea na timu kwa mzunguko wa pili ambao unakaribia kumeguka.

Pia Manara amempa pole Kaze kwa kufutwa kazi kwa kumwambia kwamba ni maisha ya soka.

Manara amesema:"Shida yenu kubwa mnataka kushindana na Simba ambayo misingi ya kitimu ishajengwa kitambo. Hamkubali kuwa Simba ni bora maradufu ya timu yenu kwa sasa.

"Hamkubali kuwa tuna management very strong, (Uongozi imara) kuwazidi mara laki, hamjawahi kuelewa, hamjawa bado na uongozi wa kushindana na bodi ya Simba.

"Pia mmekosa kiongozi au mtu kama Haji anayeweza kutoka katika public, (watu) kuwatuliza mashabiki pale hali inapokuwa tete, na hayo yote hayawezekani kufanywa katika muda mfupi kama mnavyoaminishana huko kwenu.

"Pepo tunaitaka lakini haipatikani bila kufa. Hebu shikeni haya maneno toka kwa mtu msiyempenda, siku moja yaweza kuwastiri.

"Kubalini kuwa chini yetu kwa sasa kisha mtengeneze timu na msiamini sana redio na headlines zinazowaaminisha nyie ni bora.

"Kubwa rudini nyuma mvute kasi ya kutufikia tulipo Kwa speed ya mwanariadha, hapo mlipo kukimbia kwa kushindana na Simba hamtaweza hadi kiyama.

 "Mnasajili wachezaji wasiopungua ishirini wapya kila mwaka, hii haipo kokote duniani, mbaya zaidi mnaanza kuwapamba hata kabla ya kuingia uwanjani, mnawapokea kifalme ilhali hata utumwa hawastahili," 

10 COMMENTS:

  1. kila siku tunamsikia Haji Manara akiisema Yanga na hakuna siku tulisikia viongozi wa Yanga wakiisema Simba !! tukubaliane kua kila mtu aangalie mambo yake tuache kuvurugana kisaikolojia

    ReplyDelete
  2. Manara anasahau kuwa hayo anayoyasema ya muundo wa kiuongozi yalianzia Yanga kabla ya mtu/watu fulani kutumia nguvu zao za kiutawala kuidhoofisha Yanga kwa mapenzi yao kwa upande wa pili na hata kufikia kutoa tamko hadharani kuwa Yanga kuwa bingwa ni hadi serikali ya awamu ya tano itakapoondoka madarakani
    Ilibidi mheshimiwa Kikwete atoe kauli ya kimafumbo kuwaambia hao watu kuihujumu Yanga hakutasaidia
    maana bila ya ushindani wa Yanga na Simba hakutakuwa na chachu ya maendeleo ya mpira.Wenye uwezo wa kutafakari walimuelewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Achaneni na issue za kulalamika kila wakati fanyieni kazi mapungufu yaliyopo kwenye timu

      Delete
    2. Wewe ni chizi Tena ni muongo mchonganishi Manara hajawahi kusema Yanga atachukua ubingwa mpaka Serikali hii itoke madarakani Ila nachokumbuka Mimi Malinzi aliwahi kuapa kuwa chini ya uongozi wake Simba hawawezi kuchukua ubingwa tatizo la washabiki wa Yanga wachache wasio ujua Mpira wanasingizia hujuma eti ndo zinawafanya wasichukue ubingwa mbona mnafukuza makocha Sasa Kama mnahujumiwa.Na wewe kwa akili zako zilivyokuwa finyu unafikiri Rais Magufuli na Serikali yake wanaikandamiza Yanga eti kwa sababu Manji alipata matatizo Serikali hii ilipoingia madarakani,je na sisi Simba tukisema kipindi Cha Kikwete tulikuwa tunahujumiwa utasemaje acha upumbavu tengenezi timu Simba ni timu Bora na haijajengwa kwa msimu mmoja chizi wewe

      Delete
    3. Matako ya bibi yako!!!!Ni wapi mtoa maoni ameandika kuwa Manara ndio aliesema kuwa Yanga hatachukua ubingwa mpaka serikali ya awamu ya tano iondoke madarakani.Tatizo lako unaonekana ukiwa kwenye siku zako za hedhi huwa unakurupuka kujibu bila hata ya kusoma kilichoandikwa.Manara ana nguvu gani yakiutawala katika nchi hii,inaonesha una hulka za wanawake malaya ambao hawana chembe ya aibu katika kadamnasi.Ngoja tuingie maktaba tukushushie ushuhuda wa bwana'ko fulani alietoa hiyo kauli ndo ukubali nguchiro mkubwa wew!!!
      Kipindi cha Kikwete hakuna hujuma za kijinga zilizokuwa zinafanyika baina ya hizi timu mbili isipokuwa upande wenu kulikuwa kuna mgogoro wa kimaslahi ambao uliwafanya wale waliokuwa TFF kuwakomoa wenzao walioshika timu matokeo yake mkawa mnamtuhumu bure Malinzi.

      Delete
    4. ndugu yangu tusi ulilolitoa ni maoni au ni utani maana neno hili ulilolitamka nadhani, linahitaji tafakari juu ya kile ulichokifikia, mbaya zaidi umeanza na matusi halafu unaendelea kutoa maoni chini unadhani kuna mtu atashika hayo maoni kweli? mnadhani mnapotukana hamuwezi kuchukuliwa hatua? nadhani tuanze na wewe mfano utahadithia technology imekuwa kwa speed sana msijiweke kikaangoni, kazi njema bingwa wa matusi ya mitandao

      Delete
  3. Eti wanapokelewa kifalme ili hali hata kitumwa hawastahili, duh! Kuna watu wana maneno.

    ReplyDelete
  4. Nani asiejua kuwa nyie ndio mnaoletta choko choko yanga

    ReplyDelete
  5. ikumbukwe enzi za yusufu manji yanga ilikua inatisha lakini alipopita raisi wa awamu ya tano akaingia kuharbu mipango ya yanga raisi kikwete tutamkumbuka!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic