March 8, 2021


 MWENYEKITI wa Kamati ya Ufundi ndani ya Klabu ya Yanga, Dominick Albinus amesema kuwa sababu kubwa iliyowafanya waachane na benchi lao la ufundi ni matokeo mabaya ambayo yalikuwa yakipatikana ndani ya uwanja.

Jana, Machi 7, benchi la ufundi la Yanga lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedriec Kaze, msaidizi wake Nizar Halfan, kocha wa viungo Edem Mortoisi, kocha wa makipa Vladimir Niyonkuru pamoja na Ofisa Usalama Mussa Mahundi walichimbishwa.

Mchezo wao wa mwisho ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga. Bao la Yanga lilifungwa mapema na Fiston Abdulazack likawekwa sawa na Pius Buswita dakika ya 89.

Mwenyekiti amesema:"Ilikuwa ni makubaliano kwetu na kila mmoja alikuwa anajua kwamba tunahitaji kupata matokeo na mwisho wa siku tumekuwa tukipata matokeo mabovu ambayo hayapendezi.

"Ikiwa timu haipati matokeo wa kuwatazama ni benchi la ufundi kwa kuwa wao wanatambua kwamba namna gani inahitajika kufanyika ndani ya uwanja hivyo hii ni hatua ya mwanzo na kazi inaendelea kwa wachezaji kwa kuwa nao tumewaambia kwamba wao ni sababu.

"Wachezaji tumewaambia kwamba tumeondoa benchi la ufundi kwa kuwa hakuna matokeo na ikitokea na wao pia tukagundua kwamba hakuna ambaye anajituma basi itakuwa kazi kwake," amesema.

Kaze alisaini dili jipya ndani ya Yanga Oktoba 16 baada ya kutua usiku wa Oktoba 15 huku Nizar na Edem wakitua ndani ya Yanga Januari 27 na kufutwa kazi Machi 7.

23 COMMENTS:

  1. Kocha huyo alipokewa kwa mbwembwe za namna yake lakini sasa hafai. Unajuwa ile tabia ya kwenda kuwapokea air port kila wachezaji na makocha kwa mbwembwe kubwa sana kwa kuwafikiria kuwa watafanya kazi yao kwa morali kubwa sana, jambo ndilo lililoharibu kwakuwa wengi wao wakachukulia kuwa ni watu wa kubwa na muhimu kupindukia mipaka Mpaka kujiona wana ubora kuliko mwengine yeyote na wapo huru katika kila wanalolitaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukipokewa kwa mbwebwe na wewe kazana. Ukileta ujinga unaopigwa chini

      Delete
  2. Kocha wa Barcelona ameshindwa kupata matokeo mazuri Tanzania premier league arudi zake Spain inavyoonyesha ligi ya bongo ngumu kuliko Spain huenda akija hapa real Madrid anaweza kushuka daraja pole kaze pole nizar khalifan katafute kazi kwingine

    ReplyDelete
  3. Naona yanga wamepanga kumleta pep guadiola

    ReplyDelete
  4. Walimnadi kama kocha wa Barcelona, eti kocha wa makombe..Wengine tuli mtafuta google..Barcelona alikuwa anafanya kazi tu, na Rwanda sio kivile alikuwa na ufanisi mzuri..mlimdanganya Zlatico afundishe fundishe hadi Kaze akamilishe kilicho kuwa kinamkwaza kuja Tanzania.. Kwa nini utopolo inapenda uongo uongo janja janja... Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Tambwe, morrison,Yondani na makocha Zahera, Lwandamina...hebu jaribuni kuwa wakweli...mambo mengine ni shetani tu anayoyapenda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbwembwe sio dhambi, acha kuongea pumba!

      Delete
    2. soma vizuri ..usichukue sentensi moja dhambi ni dhuruma wanazofanyiwa wachezaji Yanga..hata kama baadaye wakilipwa sio sahihi kumcheleweshea mtu masilahi yake...utajisiakiaje ukifanya kazi mwezi wa kwanza, wa pili hadi tatu bila malipo.

      Delete
  5. Kwahakika Yanga imefika wakati sasa tujicheki sisi wenyewe kwanza. Haiingii akililini hata kidogo kwa muda wa karibu mwaka tu tukabadilisha makocha karibu watano pamoja na wasaidizi wao wa hapa nyumbani. Si bure lazima iko kitu. Nyota wa mataifa wanaojulikana uwezo wao na wakifika hapa wanaonekana hawafai. Hapa, ipo kitu si bure. Yufikiri vizuri ikiwa hawa nyota waliokalifu mabilioni na sasa kuonekana hawafai, kweli baada ya mwaka tu yatatumika mabilioni mwengine kuleta nyota wapya pamoja pamoja na baraza la ufundi? Hakika inaumiza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa Kama kocha anshindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji,lazima aondoke

      Delete
  6. Kaze anamudu vzr kwenye mechi ya Simba vs yanga amepnyesha uwezo mkubwa Ila mfupa unaomshinda mbele ya timu ndogo hizi underdog Ila ameweza kushinda mbele ya azam,mtibwa sugar ila Cha kushangaza anaangukia pua kwa coastal Union dakika za mwisho na pia kwa polisi Tanzania anapata suluhu watoto wanasawazisha dakika za mwishoni kabisaa

    ReplyDelete
  7. Yanga Kuna tatizo ktk management yao Kati ya gsm na management kuu ya timu kuna walakini Sasa wakiwa wanavutana hivi ni timu ngumu kupata matokeo ya kuridhisha uwanjani

    ReplyDelete
    Replies
    1. At least wewe umeongea ki uanamichezo,lakini karibia wengine wote wanaonekana ni mashabiki maandazi....bendera fata upepo wasiojua lolote kuhusu soka.

      Delete
    2. Yawezekana uongozi una matatizo, lakini wachezajiwana tatizo gani? Uongozi ndo unamfanya mwamnyeto asiruke mipira ya vichwa? Au ndo unamwambia feisal arudishe mipira nyuma?

      Delete
  8. UTOPOLO tatizo sio kocha ila hata wachezaji wao wana waangusha haiwezekani mtu anakosa one against one

    ReplyDelete
  9. Sielewi hivi ramani yao ya ubingwa ndio ile kwenye jezi yao

    ReplyDelete
  10. Kama vipi wampe timu Senzo Mbatha Mazingisa maana walifurahi sana alivyotoka Simba kwenda Yanga,,Kuna tofauti kubwa kati ya Chungwa na Limao.Wamlete Pep Guadiola awape matokeo mazuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shida manara kawafanya Kila saa mnaongea ujinga tu

      Delete
  11. karibu wote walio comment hapa ni mashabiki wa Simba !! sasa mashabiki wa Simba wameacha kushughulika na timu yao na kujikita kwa Yanga !!

    ReplyDelete
  12. Timu imewashinda mashabiki wataandamana msolwa atoke madarakani unaonekana hata viongozi timu imewashinda haiwezekani usajili wachezaji wa gharama uje upate matokeo ya aibu Kama hayo mechi mbili pointi moja hapo bado hujakutana na Simba bado una game na namungo bado azam watatoka kweli utopolo??

    ReplyDelete
  13. Benchi la ufundi halina makosa Ila Kuna wachezaji wana shida waachwe hasa striker

    ReplyDelete
  14. Kila aina ya mchezaji walisajili kupitia headline za magazeti , sasa inakuweje wanashindwa kufikia malengo? Vp akina sarp na zilaza wenzake?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic