April 28, 2021


 BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga, Abdalah Shaibu, 'Ninja' leo anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ambacho kipo Mbeya kwa sasa.

Beki huyo hakuwa kwenye msafara uliokwea pipa jana Aprili 27 kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa Ninja anatarajiwa kujiunga na timu Mbeya baada ya kumaliza mazishi ya dada yake.

"Ninja alicheza mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam FC akiwa amefiwa hivyo aliomba amalize majukumu yake na kusafiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya msiba hivyo tayari ameshamaliza na atajiunga na timu," .

Yanga inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic