HAKUNA maisha mazuri kama yale ya kupanga kushinda kisha ukafeli kushinda kile ulichokipanga hapo nina amini kwamba kuna jambo ambalo utakuwa umejifunza.
Ni
ngumu kuamini kwamba kwenye ulimwengu wa soka zile timu ambazo zilishuka daraja
nguvu zao Ligi Daraja la Kwanza huwa inakuwa ndogo na mwisho wa siku
zinaangukia Ligi Daraja la Pili, kisha baadaye zinaanza upya kwenye Ligi ya
Mkoa.
Awali
ilikuwa ni ndoto mbaya kuota kwamba Singida United itashuka daraja na
itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kisha huko itakwama na kushushwa tena kutokana
na makosa ambayo wanaweza kuyafanya.
Ila
imekuwa hivyo sasa wao maisha yao Ligi Kuu Bara yaliwashinda, kisha wakaangukia
Ligi Daraja la Kwanza huko nako wakashindwa na kushushwa kutokana na
kushishindwa kupeleka timu uwanjani, ajabu na kweli.
Bado
sijajua timu ambazo huwa zinapanda kwa kasi na kufanya vizuri huwa zinakumbwa
na nini hasa zinapoanza kushiriki Ligi Kuu Bara.
Ninavuta
picha ile Mbeya City yenyewe ambayo ilikuwa inaishi kwenye dunia yake ya
ushindani namna ambavyo ilikuwa inaingia uwanjani kupambana na vigogo kama
Simba na Yanga.
Ile
Mbeya City ambayo shabiki wa Dar alikuwa anakubali kuvua uzi wa njano na ule
mwekundu ama ule mweusi na mweupe kisha anavaa ule wa Mbeya City.
Leo
hii mbeya City inapambana na hali yake ndani ya Ligi Kuu Bara huku ikiwa haina
uhakika wa msimu ujao kushiriki tena kwenye ligi hii labda inaweza kuangukia
Ligi Daraja la Kwanza.
Unaikumbuka
ile Mtibwa Sugar yenyewe ambayo ilikuwa ikiingia Uwanja wa Mkapa hata Uhuru
mpinzani anaanza kujiuliza mara mbilimbili namna gani anaweza kupata ushindi?
Nguvu
ilizimika ghafla baada ya timu hiyo kutwaa taji la Mapinduzi, Visiwani
Zanzibar. Iliporudi kwenye ligi mambo yakawa tofauti.
Uongozi
wa Mtibwa Sugar uliweka wazi kwamba mkwanja ambao walipewa wachezaji wao baada
ya ushindi huo uliwapumbaza na kuwafanya wasahau kuongeza juhudi, ajabu
nyingine.
Leo
hii ikiwa inapambana kutetea nafasi yake kubaki ndani ya ligi unaambiwa kwamba
kumbe Dickson Job alikuwa mhimili kwa kuwa ameondoka kaondoka na nguvu ya
ushindi.
Inawezekanaje
sasa timu bora na imara kama Mtibwa Sugar kuyumbishwa na beki? Sawa inawezekana
kwa kuwa alikuwa nahodha ila je wakati wanafanya biashara hawakatambua kwamba
ni lazima atafutwe mbadala wake.
Asanteni
sana Mtibwa Sugar kwa kuonyesha ukomavu wenu na kuendelea kupambana, bado nina
amini mashabiki wenu wanawaombea dua ili mbaki kila la kheri.
Ukirudi
kwa Ndanda FC hawa nao safari yao ya kushuka kutoka Ligi Kuu Bara ilikuwa ni
kutokana na ukata na sasa ndani ya Ligi Daraja la Kwanza mambo yamegoma tena
sababu ileile ya ukata.
Hapa
hili tatizo inabidi litafutiwe ufumbuzi na wamiliki wa timu pamoja na
Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuangalia namna ya kuzipa sapoti timu hizi.
Itazame
Njombe Mji, ilikuwa inarejea taratibu wakati ligi ilipoanza msimu huu na
matumaini yalikuwa makubwa, ghafla nayo inapambana kubaki ndani ya Ligi Daraja
la Kwanza.
Sijui
itakuaje ikiwa itashuka Ligi Daraja la Kwanza, mambo yatakuwa magumu kwa kuwa
unaambiwa lile lijalo ni gumu kuliko lile ambalo linaisha kwa wakati huu.
Wana Lipuli
bado hapo Kamwene kama haijaeleweka hivi ni muhimu kupiga hesabu upya na kuona
namna gani timu za nyanda ya Kusini zinaweza kuwa na nguvu kwenye Ligi Kuu
Bara.
Kwa
hali ilivyo ikiwa Njombe Mji haitazinduka kwa sasa naiona kule Ligi Daraja la
Pili itaungana na Boma FC ya Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara ambazo hizi zimeweka
wazi kwamba hazina nafasi ya kubaki kwenye Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment