April 10, 2021

 


HASSAN Bumbuli, Ofsa Habari wa Yanga amesema kuwa wanaosema mshambuliaji wao Ditram Nchimbi hafungi wanasahau kusema na jumla ya pasi za mabao ambazo amefunga.

Bumbuli amesema kuwa mshambuliaji huyo mzawa kwa sasa amebadilishiwa majukumu jambo ambalo linamfanya ashindwe kufunga kama ilivyokuwa zamani.

Nchimbi alisajiliwa na Yanga akitokea Klabu ya Polisi Tanzania ambapo huko alikuwa kwa mkopo akitokea Azam FC, hivyo Yanga walifanya biashara ya kumnunua mchezaji huyo ambaye alicheza pia Njombe Mji kutoka Klabu ya Azam FC.

Wakati anajiunga na Yanga, alifunga jumla ya mabao manne, hat trick aliwafunga Yanga walipokutana Uwanja wa Uhuru na bao moja aliwafunga Alliance.

Msimu huu wa 2020/21 Nchimbi hajafunga bao jambo ambalo limekuwa likizua mijadala, kuhusu hilo, Bumbuli amesema:"Wanasema kwamba Ditram Nchimbi hafungi wanasahau kwamba kazi yake imebadilika kwa sasa tofauti na awali ambapo alikuwa ni top striker kazi yake ni kumwaga majalo ili wengine wafunge,".

Februari 20, Ditram Nchimbi alitimiza mwaka mmoja wa kucheza bila kufunga bao lolote katika mechi za ushindani.

Mara ya mwisho kufunga ndani ya Ligi ilikuwa ni Februari 20,2019 Uwanja wa Mkapa ambapo alifunga mbele ya Alliance mabao mawili kwa pasi za David Molinga. 

Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 50 baada ya kufunga mabao 36 ametoa pasi mbili za mabao.

Alimpa Michael Sarpong mbele ya Biashara United na ya pili alimpa Tonombe Mukoko mbele ya Kagera Sugar. 

1 COMMENTS:

  1. Dah jamaa kageuka kocha. Hajafunga mwaka mzima ila katoa pasi 2 za magoli mwaka mzima?What a relief!
    Waksti mwingine ni bora kukaa kimya kuliko kuthibitisha ubaradhuli wako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic