Nianze na ule msemo, Milima haikutani….. Hakika ni sahihi baada ya kukutana tena na mshikaji wangu Clever Kazungu.
Huyu jamaa ni mmoja wa
waandishi wakongwe na wanaojua vizuri masuala ya soka katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati.
Anatokea Rwanda, lakini
anajua mambo mengi sana pia kuhusiana na mpira wa Tanzania hasa ukimueleza
kuanzia miaka ya 1970, 1980 anaweza kukupa stori nyingi ambazo hata wewe
ulishazisahau.
Yeye ni kati ya
waandishi magwiji wa Rwanda, hapa nyumbani wakati fulani aliwahi kufanya kazi
ya uchambuzi wa soka katika Gazeti la Championi.
Hatujakutana kwa zaidi
ya miaka sita sasa hapa Dar es Salaam, ingawa mara ya mwisho nilikutana naye
Kigali, pale Yanga ilipofunga safari kwenda Ikulu ya Rais Paul Kagame.
Karibu sana Kazungu,
najua uko kwa ajili ya michuano ya Kagame. Lakini Tanzania kwako ni nyumbani,
pia nilisikia faraja tumekutana tena.







0 COMMENTS:
Post a Comment